Featured Posts

Wednesday, June 4, 2014

USHIRIKINA WAENDELEA BONGO MOVIE, MSANII MWINGINE AAMKA NA KUKUTA AMEPIGWA CHALE ZA KUTOSHA

MWIGIZAJI mwenye figa ya aina yake Bongo Movie, Tamrina Posh ‘Amanda’ ameamka na kushtuka akiwa amechanjwa chale na watu wasiojulikana kama alivyowahi kufanyiwa marehemu Recho.

Mwigizaji mwenye figa ya aina yake Bongo Movie, Tamrina Posh ‘Amanda’.
Akizungumzia tukio hilo, Amanda alisema lilitokea siku ambayo dairekta mkongwe nchini George Tyson alipofariki dunia (Mei 30) ambapo hakujua ni nani aliyemfanyia ‘unyambilisi’ huo usiku kwani alishtuka asubuhi na kuona akivuja damu zikiashiria kuchanjwa kwa wembe.
Marehemu Recho Haule enzi za uhai wake.
“Nilijikuta nimechanjwa lakini Mungu ni mwema, waliofanya hivyo kama walikuwa na nia mbaya, wameshindwa kwani nilikwenda kuombewa kanisani halitanipata lolote,” alisema Amanda.

TUMEAMIA HUKU