Featured Posts

Wednesday, June 18, 2014

NINI KINASABABISHA AJALI BONGO MOVIE, SOMA HAPA KILICHOTOKEA JUZI

Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere akibadilisha tairi
Wasanii nyota wa filamu ‘Bongo Movie’ wakiongozwa na mwenyekiti wao Steve Nyerere wamenusurika katika ajali mbaya ya gari iliyotokea maeneo jirani na Chalinze wakiwa njiani kuelekea Dar wakitokea mjini Dodoma walipoenda kuhudhuria Tamasha la Uzalendo pamoja na Uzinduzi wa video ya wimbo wa miaka 50 wikiendi iliyopita. 

Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni kupasuka kwa matairi mawili ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Brevis lenye nambari za usajili T 200 CRY hata hivyo Hakuna mtu aliyeripotiwa kufa wala kujeruhiwa. Vicent Kigosi ‘Ray’, Shamsa Ford, Irene Uwoya, Johari na Jaccob Steven ‘JB’ ni miongoni mwa wasanii waliokuwepo eneo la tukio. 
Maisha Matamu, Johari na Shamsa Ford katika pozi, baada ya kunusurika ajalini 


TUMEAMIA HUKU