Featured Posts

Friday, June 6, 2014

MTOTO WA STAA WA BONGO MOVIE MZAA MAGARI APATA AJALI AKIENDA MSIBANI

STAA wa vichekesho, Sherry Magali ambaye pia ni mtoto wa msanii wa filamu Charles Magali amepata ajali na kuvunjika mguu alipokuwa njiani akielekea kwenye msiba wa George Otieno ‘Tyson’. 
Staa wa vichekesho, Sherry Magali akiuguza majeraha aliyoyapata baada ya ajali.
Chanzo kilichoshuhudia ajali hiyo kilieleza kuwa, ilitokea maeneo ya Sinza Kijiweni jijini Dar akiwa amepakizwa kwenye pikipiki gari ndogo iliwagonga kwa nyuma na kumfanya avunjike mguu.
Katika kujua ukweli wa tukio hilo,Sherry ambaye alisema:

Mguu wa staa wa vichekesho, Sherry Magali uliovunjika.
“Ilkuwa ajali mbaya sana, niliona roho yangu inaondoka hivihivi. Dereva hakuumia sana ila mimi niliumia na kupelekwa pale Hospitali ya Palestina, nilipopigwa X-Ray ikabainika mguu umevunjika wakanifunga hogo.”

TUMEAMIA HUKU