Featured Posts

Friday, June 20, 2014

KUSAMBARATIKA KWA PENZI LA RAY NA JOHARI KWAWAGAWA MASHABIKI

MASHABIKI wa sinema za Kibongo wamefunguka kuwa wanapenda uhusiano waliouita wa kimapenzi kati ya Wakurugenzi wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Blandina Chagula ‘Johari’.
Mwigizaji mkongwe wa tasnia ya filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’
Ishu hiyo ilijidhihirisha wazi juzikati mjini Dodoma wakati mastaa mbalimbali walipokuwa wamekwenda kuzindua video ya wimbo wa Tuulinde Utanzania katika Uwanja wa Jamhuri.
Mashabiki walidai wanapenda kuwaona wawili hao wakiwa pamoja ingawa wenyewe wamekuwa wakikanusha kuwa hawakuwahi kuwa wapenzi zaidi ya kazi.
Mkongwe wa tasnia ya filamu BongoBlandina Chagula ‘Johari’.
“Tunapenda kuona Johari na Ray wapenzi maana ni watoto wa mji wa Dodoma na tunawakubali sana,” alisema shabiki mmoja aliyetambulisha kwa jina la Ally.

TUMEAMIA HUKU