Featured Posts

Monday, June 23, 2014

HII SASA KALI EXCLUSIVE; ANGALIA HAPA PICHA AMINI AFUNGA NDOA KIMYA NA MSANII MWENZAKE


Anaweza kuingia kwenye stori za siku tena kubwa na si ukubwa wa kuoa tu ni ukubwa wa kufunga ndoa tena ikiwa ya kimya kimya bila baadhi ya mastar wenzake kuhusika na harusi hiyo ambayo wengi wamesema ilikua kama ya ghafla. 
 
Miaka kadhaa nyuma D.Knob aliwahi kufunga ndoa ya namna hii ambayo kwa maelezo yake alisema kuwa harusi yake hawakuzidi watu 15 kuanzia Kanisani mpaka sehemu waliyoamua kukaa na kupata vinywaji kadhaa.

Amini Mwinyi Mkuu kutoka THT amefata nyanyo za D.Knob na wasanii kadhaa ambao waliwahi kufuga ndoa za kimya kimya kwa Amini ndoa yake ilifungwa Msikiti wa Ibazi uliopo Manzese baada ya swala ya saa 2 usiku,idadi ya watu walioshuhudia ndoa hiyo hawakuzidi watu 20 na hiyo ni jumla ya wazazi pamoja na wasindikizaji.
 
Amini kafunga ndoa na msichana anaeitwa Farida Bashir au Namcy Vana ambaye sauti yake imesikika kwenye wimbo wa Kantangaze uliotoka miezi kadhaa iliyopita.

TUMEAMIA HUKU