Jumatano ya wiki iliyopita ndio liliibwa
hili gari aina ya BMW lisilopenya risasi
ambalo huwa linakuwepo kwenye
msafara wa Rais Kenyatta, na taarifa ya
Ikulu ilisema liliibwa wakati dereva wake
ambae ni askari alikua akielekea kwenye
makazi ya Polisi Nairobi, njiani
akasimamishwa na watu waliokuwa na
AK 47 wakamtupa mtaroni baada ya
kumvua nguo na kukimbia nalo.
Taarifa mpya ambayo inaripotiwa na
Julius Kepkoich toka Kenya inasema gari
hili limepatikana kwenye mji wa Tororo
Uganda na tayari limepelekwa Kampala
baada ya msako uliofanywa na Polisi na
kumkamata mshukiwa mmoja hotelini
mjini Bungoma.
Kikosi cha Polisi wa Flying squard
kikishirikiana na Interpol walivuka boda
na kuingia mji wa Tororo Uganda
walikohisi kwamba ndiko kulikopelekwa
gari hilo.
Polisi wanamshikilia Nelson Topicho
aliyekamatwa Bungoma na anatarajiwa
kurejeshwa Nairobi ili kuhojiwa zaidi
ambapo kikosi kingine cha Nakuru Kenya
kinamshikilia Agrey Odhiambo
anaetuhumiwa kukarabati gari lililoibwa
na kumiliki bunduki huku Nairobi
wakitarajiwa kumuhoji upya dereva wa
Ikulu David Muchui.