Featured Posts

Saturday, September 6, 2014

WASTARA.AFUNFISHWA. KUVAA NUSU UTUPU

WIKI iliyopita tuliishia pale mwigizaji Wastara Juma
alipokuwa akimwelezea mchumba wake wa pili
alivyokuwa hajatulia kiasi cha kumchanganya na
wanawake watatu tofauti. Leo anaelezea
alivyokutana na majanga mengine kwa mwanaume
mwingine.
“Huyu mwanamke wa tatu baada ya kuondoka
niliomba namba yake kwa mdogo wake huyo
mchumba, nikampigia na kumuomba nionane
naye. Bila hiyana alinikubalia, nilipoonana naye
ndipo akanipasulia siri zote za yule mwanaume,
iliniuma sana.
“Kutokana na ubishi wangu, nikawa kama
siaminiamini, akaniambia kama siamini niende
kuangalia albamu yake ambapo niliporudi kwao
niliangalia albamu yake na kukuta picha akiwa na
wanawake tofauti tena kimahaba, nilipotoka hapo
sikurudi tena na aliponitafuta kwa simu
nilimwambia simuhitaji tena.
Mwandishi: Baada ya kuachana na huyo mchumba
ulimpata mwingine?
“Ndiyo nilikutana na mwanaume anaitwa Kushi
ambaye hatukuchunguzana muda mrefu tukaoana,
baada ya ndoa niligundua kwamba ni mlevi
kupindukia, siyo mwaminifu na alikuwa mkorofi
sana hivyo wiki moja baada ya ndoa tulipigana
sana baa.
“Alikuwa akioa asubuhi na jioni kwani ndani ya
ndoa yangu alioa wanawake watano na kuwaacha,
alikuwa ni tajiri sana lakini alipenda starehe
kupindukia hakuwa akinijali hata nguo ya ndani
nilikosa nilikuwa navaa zilizochanika, nakumbuka
nikiwa na ujauzito aliniambia maisha ni magumu
niende nyumbani kwetu nirudi baada ya wiki mbili
atakuwa ameshapata hela ya kodi ya nyumba.
“Wiki mbili nilizomuacha alioa mwanamke
mwingine ambaye waliachana baada ya siku
chache na kwenda Bagamoyo kwa mwanamke
mwingine, maisha yake yakawa ndiyo hayo.
“Siwezi kumsahau huyu mwanaume na sitaki
kumsikia kwa sababu aliniharibia dira nzima ya
maisha yangu kwani kwake ndipo nilianza kuvaa
suruali, kwenda klabu na baa wakati kabla ya hapo
nilikuwa sivijui kabisa vitu hivi, alikuwa hataki niwe
na marafiki akiona nina rafiki wa kike anatembea
naye, kutokana na mateso hayo ilipofika mwaka
2001 tuliachana ikiwa ni baada ya kuishi kwa
mwaka mmoja tu katika ndoa.
Mwandishi: Je nini kiliendelea baada ya kuachana
na Kushi?
“Nilianza maisha yangu mwenyewe mpaka mwaka
2003 nikakutana na Msafiri Kondo (Solo Thang)
ambaye tulikutana kwenye kazi baada ya tamasha
ndiyo tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi kwa
muda mfupi nikapata ujauzito ndipo akarudi Kushi
na kuomba msamaha.
“Alipoona nakataa kumsamehe akachunguza niko
na nani akagundua ndipo alipomfuata Msafiri na
kumtishia kwamba atamloga, nikamwambia Msafiri
asihofu lakini akawa bado ana wasiwasi lakini naye
sikumchunguza sana kabla kwani nilikuja
kugundua kwamba alikuwa na mwanamke
mwingine.
“Nilijifungua mtoto akiwa na siku tano Msafiri
alisafiri na kwenda Ulaya ambako huko alioa na
kuzaa watoto wawili hivyo akawa ananitumia
matumizi ya mtoto mara mojamoja kwa hiyo
kuanzia hapo nikawa nawalea wanangu wawili
mwenyewe.
“Nilikaa mwenyewe na wanangu kuanzia mwaka
2004-2006 ambapo mwaka 2006 nilirudi rasmi
kwenye sanaa ya filamu kwani mwanzoni nilifanya
nikiwa shuleni.Wastara amezungumza vitu vingi
kuhusu maisha yake. Usikose sehemu ya mwisho
ya makala haya wiki ijayo!

TUMEAMIA HUKU