Mwaka 2013 ni watu wachache tu waliokuwa
wakilifahamu jina la Nuh Mziwanda kwakuwa
alikuwa msanii mchanga anayetafuta nafasi yake
kwenye muziki wa Tanzania. Wimbo wake ulioanza
kumtambulisha uliitwa ‘Otea Nani’ ambao ulipata
nafasi kiasi kwenye vituo vya redio.
Lakini jina la muimbaji huyo lilikuja kuwa kubwa
zaidi baada ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi
na Shilole, uhusiano ambao umekuwa wa wazi
katika mitandao yao ya kijamii. Kuonesha kuwa
ana mapenzi ya kweli kwa Shilole ambaye ni
mama wa watoto wawili, Nuh alijichora tattoo
mkononi yenye jina la Shilole.
Shilole pia aliamua kumpa shavu mpenzi wake kwa
kuonekana kwenye video ya wimbo wake
‘Msondongoma’ na hivyo kumwongezea wigo
zaidi. “Yeye ndo Mama watoto Mungu akijaalia,”
aliandika Nuh kwenye picha ya Shilole aliyoiweka
kwenye akaunti yake mtandao wa Instagram yenye
followers zaidi ya 19,000.
“Ukichagua kitu roho yako inapenda raha
sana.sasa kwa mfano mimi Mziwanda nna haja
gani ya kucheat wakati mtoto ana kila kitu,
kiukweli napenda mke wangu alivyojaa jaa mie
hoooooi,” aliandika kwenye picha nyingi ya
Shilole.
Naye Shilole kwenye picha aliyoiweka kwenye
mtandao huo akiwa na Nuh Mziwanda aliandika,
“Ilove my baby,” kudhihirisha upendo wake.
Hakuna shaka kuwa uhusiano huo umemwezesha
Nuh Mziwanda kukuza jina lake na ameutumia
vizuri kujitambulisha zaidi.