Yupo kwenye orodha ya Wasanii ambao wanazo rekodi zao kwenye chati ya muziki wa bongofleva Tanzania na nchi jirani zinazocheza muziki wa kiswahili ambapo baada ya miaka kadhaa ya kuifanya bongofleva aliamua kuhamia Kenya kutafuta mkwanja zaidi pia kuuongezea muziki wake ladha nyingine.
Sasa hivi ataonekana sana kwenye kioo chako baada ya kutoa hii video mpya aliyoifanya Kigali Rwanda ambapo jina la video lilikua liwe ‘nimepona’ ila jamaa wakakosea na kuiandika ‘mimi na wewe’ ila sio kesi.
Hussein Machozi amesema alipata nafasi ya kuifanya video hii kwenye nyumba ya Rais Paul Kagame kirahisi sababu producer wa hii single ni Mrwanda na hata yeye mwenyewe Hussein ana asili ya Rwanda kwa upande wa mama mzazi, hivyo vyote vimesaidia kwake kupata nafasi hiyo.
Rais Paul Kagame ambae ni miongoni mwa Marais wanaopenda sana kuwasaidia vijana ambae pia ana rekodi za kusaidia hata Wasanii wa nchi yake, huwa haishi kwenye hii nyumba bali familia yake.
President Kagame aliwahi pia kumsaidia mmoja kati ya Wasanii vijana wa Rwanda lakini mwaka huu msanii huyo ameingia kwenye kashfa ya kutaka kuipindua nchi ikiwemo kumpindua madarakani Rais Paul Kagame mwenyewe.
Ukishaitazama hii video mpya ya Hussein Machozi hapa chini unaweza kuacha maoni yako ili jioni saa moja akiingia akutane na comments za mashabiki wake.
Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam
-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392
milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa
ajili y...