Featured Posts

Sunday, September 21, 2014

BAADAYA KUOLEWA NA MZUNGU, LUCY KOMBA AANZA KUWAPONDA WANAUME WA KIBONGO

Stori: Imelda Mtema
MAKAVU! Msanii aliyefunga pingu za maisha juzikati na mwanaume mwenye asili ya Denmark, Janus Stanley Landrock, Lucy Komba amesema kadri siku zinavyozidi kwenda anazidi kunogewa na mapenzi ya mzungu wake na kuwaona Wabongo si lolote kutokana na kuwa waongo.
Msanii wa Bongo Muvi , Lucy Komba akiwa na mume wake mdenmark, Janus Stanley Landrock.
Akieleza la rohoni mbele ya paparazi wetu, Lucy alisema anatamani angefahamiana mapema na mzungu huyo kuliko kuyumbishwa na mapenzi ya Kibongo ambayo yamejaa ahadi nyingi za uongo, tofauti na watu wa asili hiyo ambao wana msimamo mkubwa katika mapenzi.
“Nilipopataka siyo siri nimefika, kama ulaghai nishakumbana nao sana katika mapenzi ya Kibongo ambayo yalinikinaisha mno, lakini sasa sina mawazo kabisa katika haya mambo, wenzetu hawapendi kuchepuka hovyo akikupenda, anakupenda kweli,” alisema Lucy.

TUMEAMIA HUKU