Mashabiki wa Apple Ijumaa hii wamezishika simu zao mpya za iPhone 6 baada ya kungojea kwa siku kadhaa nje ya maduka yanayouza simu. Hata hivyo, zaidi ya iPhones milioni 5 zinaweza kuishia kwenye soko haramu la Kichina ambapo zinaweza kuuzwa kwa bei mara tatu zaidi. Jijini London Ijumaa hii mamia ya watu walikuwa wamejipanga kwenye mistari mirefu huko Covent Garden na Regent Street walionekana wakisherehekea kila baada ya kupata simu zao.
Sam Sheikh, 27, anayeishi London, amedai kuwa amesubiria kwa siku tatu kungoja siku yake na amekuwa mteja wa kwanza wa Uingereza kupata simu
Wakati huo huo huko Marekani kwenye duka la Birmingham kulikuwa na msululu mrefu wa zaidi ya mita 100 ambapo simu zote ziliisha ndani ya dakika 10 tu. Simu hizo zinauzwa kwa kuanzia £539 kwa zile zenye GB16, £619 kwa zile zenye GB 64 na £699 kwa simu zenye GB 128. iPhone 6 Plus zinauzwa kwa kuanzia £619 kwa ile yenye 16GB, £699 kwa yenye 64GB na £789 yenye 128GB.