Ben Pol ni msanii ambaye amekuwa nadra kuingia
kwenye headlines zinazohusu mapenzi ya mastaa
wa bongo na pia ni miongoni mwa wasanii
wasioweka hadharani mahusiano yao ya
kimapenzi.
Lakini safari hii muimbaji huyo wa ‘Unanichora’
amepost picha iliyozua maswali mengi, lakini yote
yakihitaji jibu moja tu, ‘Huyu ndiye ‘baby’ wa Ben
Pol?
Katika picha Ben Pol anaonekana kifua wazi huku
pembeni yake yupo mrembo aitwaye Latifah
Mohamed aliyekuwa mshindi wa pili katika Miss
Tanzania 2013.