Nguvu ya vyombo vya habari ndio iliyowapelekea
Kim Kardashian na Kanye West kupata jina la binti
yao sababu wanandoa hao hawakubuni jina la
‘North’.
Rapper Kanye West na mke wake Kim Kardashian
mwaka jana waliwashangaza watu wengi kwa
kuamua kumpa mtoto wao wa kike jina la ‘North’,
ambalo kidogo lilionekana kuwa tofauti. Lakini
haikuwahi kufahamika wapi lilikotokea wala sababu
za kuamua kumpa jina hilo.
Mitandao mingi ilianza kuandika juu ya tetesi za
jina la mtoto wa couple hiyo ni ‘North’, na huo
ndio ulikuwa mwanzo wa Kanye na Kim kuanza
kulifikiria na mwisho wa siku wakalipitisha.
Kim Kardashian ameutoa ukweli huo katika
mahojiano na jarida la GQ:
“Ilikuwa ni uvumi kwenye vyombo vya habari, na
sisi hatukulichukulia kiumakini kabisa jina la North.
Lakini Kanye na mimi tulikuwa tunapata chakula
cha mchana na Pharrell akaja tulipo akasema, ‘Oh
my God, mmemua kweli kumuita mtoto wenu
North? Hilo ni jina zuri sana.”
“Baada ya muda kupita Anna Wintour alikuja na
kutuuliza kitu hicho hicho, alituambia ‘North is a
genius name. Kanye na mimi tukatazamana na
kucheka” Alisema Kim
Baada ya hapo ndio waliamua kulipitisha jina la
‘North’ kwa mtoto wao wa kwanza wa kike.