Kama mwanaume lazima upate wakati
wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili
ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
USAFI BINAFSI
Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda
sana usafi. Ni aghalabu sana kukutana na
mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana
wanaitwa mapambo ya nyumba au la
nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya
kupenda sana usafi.
Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume
mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini
kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako,
lazima uishi katika nyumba safi. Hata
anapokuja kukutembelea, anakuta
mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi
chumbani.
Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa
rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta
na kuendelea mbele.
KUJIAMINI
Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na
mwanaume ambaye anajiamini – mwenye
uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza
sawia. Siyo anayebabaika. Suala la msimamo
binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko
hata kumnunulia manukato mapya!
Mathalani unakuwa naye katika mtoko,
angependa kukuona ukiwa katika hali halisi
ya maisha yako, usiyeyumbishwa na
mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza
kukupima hata katika jambo ambalo
amekosea yeye, ataangalia unavyotoa
maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona
kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote.
Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na
matege wala makengeza!
KUJITETEA
Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana
na kilichopita, lakini hapa ni kwenye
upande wa kujitetea zaidi. Wakati unapodai
haki yako mbele ya mwanamke wako, suala
la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume
ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka
wenye uwezo wa kusimama kidete kuona
haki zao hazichukuliwi kirahisi.
Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee
kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia
haki ya mwanamke wako. Nisieleweke
vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni
yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi
na ambaye yupo tayari kwa lolote!
Inapowezekana, uwe na uwezo wa
'kuzichapa' ikiwa mtakutana na vibaka au
watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/
kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.
Mwanaume aliye 'fiti' ni chaguo la
wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole
kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu
hana nafasi.
KUJALI
Wanawake wanapenda sana wanaume
wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na
wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna
tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya
kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi
wako kwa kila hali.
Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua
maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa
sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano
hai.
UKARIBU
Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha
mkubwa wanawake ni pamoja na
kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye
katika mambo mengi unayoyafanya kila
siku.
Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka
kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo
au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo
madogo sana lakini yanayoongeza nakshi
katika mapenzi.
Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya
utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu
yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze
kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa!
KUMSIFIA
Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama
ni jambo lisilo na maana sana kwao na
wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa
wanawake ambao hupenda kuwasifia
wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya
namna wanandoa wa jinsia mbili tofauti
wanavyotambulishana kwa jamaa zao.
MWANAUME: "Peter kutana na mke wangu,
anaitwa mama Diana. Nipo naye mwaka wa
tatu sasa, tuna watoto wawili, huyo Diana
na mwingine anaitwa Cris. Mama Diana,
huyu ni Peter nilisoma naye A – Level,
Tosamaganga Sekondari."
MWANAMKE: "Suzan, huyu ndiye mume
wangu mpenzi...anaitwa Elifaraja lakini
mimi napenda zaidi kumuita Elly. Kiukweli
nampenda sana mume wangu jamani, tuna
mtoto wetu mmoja, anaitwa Agness.
(Akimgeukia mumewe) Baby, huyu hapa ni
rafiki yangu Suzan. Yaani tumekua naye
mtaa mmoja huko Arusha."
ANGALIA TOFAUTI
Bila shaka kwa namna wawili hao
walivyotambulishana unaweza kuona
tofauti kubwa. Mwanaume
amemtambulisha mkewe kawaida kabisa,
hajaonesha manjonjo au namna
anavyompenda na kumthamini mwenzake,
lakini mwanamke amefanya hivyo.
Sikia nikuambie, KUMSIFIA mwanamke,
kuna nafasi kubwa sana kwake. Chunguza
kwa makini, hata kunapokuwa na
mgongano katika familia, halafu wakatokea
wageni, baada ya utambulisho na
mazungumzo ya hapa na pale, wageni
wakiondoka kunakuwa na uwezekano
mkubwa zaidi wa kumaliza mpasuko katika
familia.
Jenga utamaduni wa kumsifia mpenzi
wako, unamuweka katika kilele cha
upendo. Anajiona kamili, peke yake na
mwenye nguvu kwako. Anajiamini na
unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa
anaamini yupo na mwanaume ambaye
anajivunia kuwa naye.
MALENGO
Wanaume wengi wana ulemavu mmoja;
hawapendi kuwashirikisha wanawake
katika mambo yao. Wanapenda kufanya
mambo yao kwa siri na wakati mwingine
ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa
mshtukizo baada ya kukamilisha jambo
husika.
Hii si sahihi. Dunia ya leo imebadilika rafiki
zangu. Inawezekana wazee wa zamani
walikuwa sahihi, maana ilikuwa ni suala la
kununua ng'ombe na kuwaweka katika zizi
kwenye kijiji cha jirani, halafu wanapewa
malisho mazuri, baada ya miaka miwili
wanazaliana, hapo ndipo anamweleza
mkewe.
Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo
mengi. Kuna suala la hasara katika biashara,
utapeli n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa
kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu
zaidi kuliko yeyote. Yes! Mkeo ndiye ndugu
yako maana umetengeneza naye familia.
Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga
maisha pamoja.
Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye
mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu
ya malengo yako, wakati mwingine
anaweza kukusaidia sehemu ambayo
hukutarajia.
Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo
yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona
mama katika familia yenu. Msaidizi kamili
wa nyumba yenu.
KIPAUMBELE
Kuna wakati wanawake huwa na mambo
yao binafsi. Kazini au kifamilia.
Inawezekana akatatizika katika eneo fulani
ambalo kwa namna moja ama nyingine
atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo
akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia,
amekuambia mmoja wa wazazi wake
anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini
kuonesha kujali kwako tu, kutampa
matumani kwamba anaishi na mtu sahihi.
Acha kupuuza mambo yake; hata yale
madogo, kama ya 'mtoto wa dada
amerudishwa ada shuleni'.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo
na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika
upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una
tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia,
mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo
uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa
kumshirikisha likawa jepesi zaidi na
mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele
kwa namna yoyote ile, kunaongeza
mapenzi zaidi kwa mwanamke.
TENDO LA NDOA
Hiki ni kipengele nyeti, kinachohitaji lugha
nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna
siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi
cha ndoa. Maana hata maandiko yanasema:
"Mwanamke ataacha wazazi wake na
kwenda kwa mumewe, nao watakuwa
mwili mmoja."
Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni
muhimu likaheshimiwa na kutengewa
muda maalum wa kufurahia. Si papara. Kwa
bahati mbaya wanaume huwa si
wafuatiliaji sana wa kujua namna ya
kuwafurahisha zaidi wenzao. Wenyewe
wanajiwazia wenyewe. Wanafikiria namna
ya kuwakomoa wenzao.
Si sahihi.
Tendo la ndoa halina maana ya
kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya
maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza
hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke
wako katika eneo hili, ni wazi kwamba
utazidisha upendo wake kwako, lakini pia
atakuwa katika kuta za uaminifu. Akatafute
nini nje wakati wewe ndiye mganga wake
unayeweza kumtibu barabara?
Kuna kitu nimesahau kweli? Kama kipo
nitafute pembeni, kwa hapa haya yatoshe
kukufanya uelewe nilichotaka kukuelekeza.
Nikuache na neno moja; uamuzi
wa kuijenga ndoa yako upo mikononi
mwako. Ukitaka iwe shaghalabaghala, pia
ni wewe tu!
Kama mwanaume lazima upate wakati
wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili
ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
USAFI BINAFSI
Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda
sana usafi. Ni aghalabu sana kukutana na
mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana
wanaitwa mapambo ya nyumba au la
nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya
kupenda sana usafi.
Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume
mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini
kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako,
lazima uishi katika nyumba safi. Hata
anapokuja kukutembelea, anakuta
mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi
chumbani.
Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa
rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta
na kuendelea mbele.
KUJIAMINI
Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na
mwanaume ambaye anajiamini – mwenye
uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza
sawia. Siyo anayebabaika. Suala la msimamo
binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko
hata kumnunulia manukato mapya!
Mathalani unakuwa naye katika mtoko,
angependa kukuona ukiwa katika hali halisi
ya maisha yako, usiyeyumbishwa na
mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza
kukupima hata katika jambo ambalo
amekosea yeye, ataangalia unavyotoa
maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona
kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote.
Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na
matege wala makengeza!
KUJITETEA
Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana
na kilichopita, lakini hapa ni kwenye
upande wa kujitetea zaidi. Wakati unapodai
haki yako mbele ya mwanamke wako, suala
la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume
ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka
wenye uwezo wa kusimama kidete kuona
haki zao hazichukuliwi kirahisi.
Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee
kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia
haki ya mwanamke wako. Nisieleweke
vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni
yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi
na ambaye yupo tayari kwa lolote!
Inapowezekana, uwe na uwezo wa
'kuzichapa' ikiwa mtakutana na vibaka au
watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/
kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.
Mwanaume aliye 'fiti' ni chaguo la
wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole
kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu
hana nafasi.
KUJALI
Wanawake wanapenda sana wanaume
wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na
wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna
tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya
kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi
wako kwa kila hali.
Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua
maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa
sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano
hai.
UKARIBU
Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha
mkubwa wanawake ni pamoja na
kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye
katika mambo mengi unayoyafanya kila
siku.
Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka
kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo
au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo
madogo sana lakini yanayoongeza nakshi
katika mapenzi.
Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya
utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu
yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze
kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa!
KUMSIFIA
Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama
ni jambo lisilo na maana sana kwao na
wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa
wanawake ambao hupenda kuwasifia
wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya
namna wanandoa wa jinsia mbili tofauti
wanavyotambulishana kwa jamaa zao.
MWANAUME: "Peter kutana na mke wangu,
anaitwa mama Diana. Nipo naye mwaka wa
tatu sasa, tuna watoto wawili, huyo Diana
na mwingine anaitwa Cris. Mama Diana,
huyu ni Peter nilisoma naye A – Level,
Tosamaganga Sekondari."
MWANAMKE: "Suzan, huyu ndiye mume
wangu mpenzi...anaitwa Elifaraja lakini
mimi napenda zaidi kumuita Elly. Kiukweli
nampenda sana mume wangu jamani, tuna
mtoto wetu mmoja, anaitwa Agness.
(Akimgeukia mumewe) Baby, huyu hapa ni
rafiki yangu Suzan. Yaani tumekua naye
mtaa mmoja huko Arusha."
ANGALIA TOFAUTI
Bila shaka kwa namna wawili hao
walivyotambulishana unaweza kuona
tofauti kubwa. Mwanaume
amemtambulisha mkewe kawaida kabisa,
hajaonesha manjonjo au namna
anavyompenda na kumthamini mwenzake,
lakini mwanamke amefanya hivyo.
Sikia nikuambie, KUMSIFIA mwanamke,
kuna nafasi kubwa sana kwake. Chunguza
kwa makini, hata kunapokuwa na
mgongano katika familia, halafu wakatokea
wageni, baada ya utambulisho na
mazungumzo ya hapa na pale, wageni
wakiondoka kunakuwa na uwezekano
mkubwa zaidi wa kumaliza mpasuko katika
familia.
Jenga utamaduni wa kumsifia mpenzi
wako, unamuweka katika kilele cha
upendo. Anajiona kamili, peke yake na
mwenye nguvu kwako. Anajiamini na
unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa
anaamini yupo na mwanaume ambaye
anajivunia kuwa naye.
MALENGO
Wanaume wengi wana ulemavu mmoja;
hawapendi kuwashirikisha wanawake
katika mambo yao. Wanapenda kufanya
mambo yao kwa siri na wakati mwingine
ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa
mshtukizo baada ya kukamilisha jambo
husika.
Hii si sahihi. Dunia ya leo imebadilika rafiki
zangu. Inawezekana wazee wa zamani
walikuwa sahihi, maana ilikuwa ni suala la
kununua ng'ombe na kuwaweka katika zizi
kwenye kijiji cha jirani, halafu wanapewa
malisho mazuri, baada ya miaka miwili
wanazaliana, hapo ndipo anamweleza
mkewe.
Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo
mengi. Kuna suala la hasara katika biashara,
utapeli n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa
kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu
zaidi kuliko yeyote. Yes! Mkeo ndiye ndugu
yako maana umetengeneza naye familia.
Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga
maisha pamoja.
Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye
mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu
ya malengo yako, wakati mwingine
anaweza kukusaidia sehemu ambayo
hukutarajia.
Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo
yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona
mama katika familia yenu. Msaidizi kamili
wa nyumba yenu.
KIPAUMBELE
Kuna wakati wanawake huwa na mambo
yao binafsi. Kazini au kifamilia.
Inawezekana akatatizika katika eneo fulani
ambalo kwa namna moja ama nyingine
atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo
akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia,
amekuambia mmoja wa wazazi wake
anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini
kuonesha kujali kwako tu, kutampa
matumani kwamba anaishi na mtu sahihi.
Acha kupuuza mambo yake; hata yale
madogo, kama ya 'mtoto wa dada
amerudishwa ada shuleni'.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo
na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika
upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una
tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia,
mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo
uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa
kumshirikisha likawa jepesi zaidi na
mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele
kwa namna yoyote ile, kunaongeza
mapenzi zaidi kwa mwanamke.
TENDO LA NDOA
Hiki ni kipengele nyeti, kinachohitaji lugha
nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna
siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi
cha ndoa. Maana hata maandiko yanasema:
"Mwanamke ataacha wazazi wake na
kwenda kwa mumewe, nao watakuwa
mwili mmoja."
Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni
muhimu likaheshimiwa na kutengewa
muda maalum wa kufurahia. Si papara. Kwa
bahati mbaya wanaume huwa si
wafuatiliaji sana wa kujua namna ya
kuwafurahisha zaidi wenzao. Wenyewe
wanajiwazia wenyewe. Wanafikiria namna
ya kuwakomoa wenzao.
Si sahihi.
Tendo la ndoa halina maana ya
kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya
maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza
hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke
wako katika eneo hili, ni wazi kwamba
utazidisha upendo wake kwako, lakini pia
atakuwa katika kuta za uaminifu. Akatafute
nini nje wakati wewe ndiye mganga wake
unayeweza kumtibu barabara?
Kuna kitu nimesahau kweli? Kama kipo
nitafute pembeni, kwa hapa haya yatoshe
kukufanya uelewe nilichotaka kukuelekeza.
Nikuache na neno moja; uamuzi
wa kuijenga ndoa yako upo mikononi
mwako. Ukitaka iwe shaghalabaghala, pia
ni wewe tu!