MAJANGA! Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na muigizaji Adam Haji ‘Baba Haji’ nusura wazichape baada ya kupishana kauli.
‘Uwanja wa vita’ ulikuwa ni kwenye msiba wa mwigizaji mwenzao Sheila Haule ‘Recho’, Sinza-Palestina, jijini Dar ambapo chanzo kilishuhudia mtiti huo, kilidai tatizo liliibuka mara baada ya Steve Nyerere kumchimba mkwara Baba Haji asijiweke karibu na Jacob Steven ‘JB’.
“Hata haikujulikana kwa nini Steve hakutaka Baba Haji awe karibu na JB, akammaindi ndipo mtiti ulipoibuka, wakataka kushikana mashati bahati nzuri Mtitu (William) akawaamua,” kilieleza chanzo.
Akizungumzia sakata hilo baada ya kutulizwa ‘munkari’, Baba Haji alisema anamshangaa Steve kwa kumchimba mkwara asikae na JB pasipo kuwa na sababu za msingi.
Akizungumzia sakata hilo baada ya kutulizwa ‘munkari’, Baba Haji alisema anamshangaa Steve kwa kumchimba mkwara asikae na JB pasipo kuwa na sababu za msingi.