Featured Posts

Saturday, May 24, 2014

HAYA NDIYO YALIKUA MANENO YA MWISHO YA MSANII 2PAC SIKU ALIPOPIGWA RISASI

Screen Shot 2014-05-24 at 6.36.29 PM
Kabla ya kuuwawa, hapa ni wakati Tupac akiondoka Mahakamani New York
Alizaliwa June 16 1971 huko New York Marekani na kufariki September 13 1996 Las Vegas Nevada Marekani baada ya kupigwa risasi zilizosababisha apelekwe University Medical Center of Southern Nevada lakini akafariki dunia siku sita baadae.
Sasa taarifa za hivi karibuni zilizotolewa na Chris Carroll ambae ni askari polisi aliewahi kwenda kwenye eneo la tukio Tupac alipopigiwa risasi, zinasema maneno ya mwisho yaliyotolewa na rapper huyu ni ‘F**k you’ na alitoa hilo tusi akiwa mikononi mwake.
Carroll anasema alijaribu kumuuliza Tupac mara kadhaa ili amwambie anahisi ni nani alihusika kwenye shambulio hilo la kumpiga risasi? mwishowe ndio akatoa hilo tusi kabla ya kuchukuliwa na kupelekwa hospitali.
Kila kinachonifikia ni haki yako ukipate mtu wangu na kama hupendwi kupitwa unaweza kujiunga na mimi kwenye mitandao ya twitter facebook na Instagram kwa kubonyezaTWITTER FACEBOOK INSTA ili niwe nakutumia kila kinachonifikia.

TUMEAMIA HUKU