Wasanii wasioishiwa vituko Tanzania, Miss Ruvuma 2005 Isabela Mpanda na Luteni Karama wameonekana katika viwanja mbalimbali vya burudani wakipeana mahaba momoto na kudai kuwa wanawakomesha waliotia doa mapenzi yao na kusababisha yasambaratike....
Isabela na Karama ambao waligombana na kutengana kabisa kwa madai kuwa Karama siyo mwaminifu katika mapenzi yao walifikia hatua mbaya ya kurushiana matusi lakini sasa hivi wamerudiana na kuwaacha midomo wazi waliokuwa wakishabikia ugomvi wao.....
"Sina la kuongea kabisa, nilikuwa sina raha kabisa maishani mwangu, nilikuwa natumiwa meseji za ajabu lakini niliomba Mungu hatimaye Karama amerudi katika himaya hii, hapana chezea Bella" Alisema Isabella
Aliongeza kwa kusema kuwa yeye kama Bella ameamua kutulia na Karama kwa sababu ameona michepuko siyo dili na inaweza kumharibia maisha yake na watoto....
Hata hivyo baadhi ya marafiki wa Bella wamedai kuwa hivi sasa Karama amefika kwa Bella kwani haendi katika mishemishe zake za kila siku kwa madai kwamba anamtuliza mpenzi wake aliyekuwa na ugomvi naye