Ukiwa umepita mwezi mmoja tangu msanii wa Tasnia ya Filamu anayejulikana kwa jina la Isabella Francis 'Vai wa Ukweli' kuripotiwa kujiuza, sasa msanii huyo amekumbwa na kashfa nyingine ya kupiga picha za uchi zikimuonesha akivua nguo mbele ya wanaume....
Akiongea na mpekuzi wetu, mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Bonny alisema picha hizo zimetawala kwenye mitandao ya kijamii hali inayozidi kumuweka pabaya msanii huyo katika ushiriki wa kazi za klabu ya Bongo Movie Unity yenye uongozi mpya ambayo imekemea vitendo visivyoendana na maadili ya kitanzania....
Bonny alisema picha hizo aliuziwa na jamaa mmoja kwa kurushiwa kwenye simu kwani yeye amekuwa na utaratibu wa kukusanya picha za mastaa waliokuwa katika pozi na kuzihifadhi kwenye simu yake....
"Lakini kinachoniuma ni kwamba huyu binti namjua tangu akiwa mdogo na amewahi kuwa mshikaji wangu,nimewahi kumshauri aachane na huo ujinga wa kupiga picha zisizo na maadili lakini amekuwa hanisikii,safari hii nimezifuma picha hizi alizopiga akiwavulia nguo wanaume kibao waliokuwa wakimtazama bila aibu" Alisema Bonny
Aliendelea kusema picha hizo mbali ya kuonyesha sehemu zake muhimu lakini zinakiuka heshima ya mwanamke ambapo anatakiwa kujihifadhi sehemu nyeti ambazo zinastahili kuonwa na mtu wake wa karibu tu..
Kufuatia kukithiri kwa vitendo vya kikahaba katika kundi la Bongo Movie Unity, uongozi mpya uliochini ya Steve Nyerere umetoa tahadhari kwa wanachama wake watakaoshiriki mambo yaliyokinyume na maadili....