Jeneza lenye mwili wa Adam Kuambiana.
Habari kutoka kwa mtu wa karibu na Kuambiana zinasema kuwa, Ijumaa (siku moja kabla ya kifo chake) alionekana baa mbalimbali akizungumza na mashabiki wake, jambo lililoashiria kuwa ni kama alikuwa akiwaaga.
Adam Kuambiana.
“Alikwenda Shikamoo Pesa (Sinza Kwaremmy), Green Park (Mwenge), New Sinza (Kwa Remmy) Igo (Sinza Mori) ambapo alikaa hadi usiku wa manane. Alionekana mchangamfu sana na alizungumza na watu wengi sana siku hiyo. Ni kama alijua angekufa ndiyo maana akaamua kuagana na mashabiki wake,” alisema.