JESHI la polisi mkoa Kigoma limefanikiwa kukamata silaha za kivita aina ya SMG, mabomu matatu ya kutupa kwa mkono, risasi 64 pamoja na kuwauwa watu watano wanaosadiliwa kuwa ni majambazi wakati wa purukushani za majibizano baina majambazi hao na askari polisi mkoani Kigoma.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani humo kamishina msaidizi wa polisi mkoa kamanda Japhal Ibrahim alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:45 alfajiri Septemba 3 mwaka huu, katika barabara kuu ya Kasulu – Kibondo eneo la pori la Malagalasi Wilayani Kasulu.
|