Mwanadada Hadija Seif (Dida’s Fashion) aliyekuwa mke wa ndoa wa msanii wa muziki Q Chillah amefunguka kisa kilicho afanya waachane pamoja na jitihada alizozifanya kumnusuru msanii huyo na wimbi la matumizi ya madawa ya kulevya.
Akizungumza katika kipindi cha Mboni Show, akiwa nchini Uingereza, Dida alisema Q Chillah ndiye aliyemtumia ujumbe wa kumwacha.
“Nilimpigia simu akaniambia ‘najua wewe haupo Uingereza unanidanganya’ ,nikamwambia ‘nipo UK’,'akaniambia upo UK’? Hii code namba ya nchi gani?’, ‘nikamwambia kwani vipi?’Kuna muda kadi huwa zinatokea hivyo akakasirika akaniambia ‘upo kwa bwana yako’,nikamwambia ‘mimi siko huko’, nikawasiliana na baba yake mzee Katwila nikamwambia ‘baba, Q Chillah ananimbia hii namba siyo sahihi nifanyeje?’, baba yake mzee Katwila akaniambia ‘usiwe na wasiwasi mimi nitayamaliza’. Ile hasira yake akampigia mama yangu kwakuwa yeye anapatana sana mama yangu. Kwahiyo akaenda akamlilia mama yangu, akamwambia mimi nimetoka nimeenda kwa wanaume sijui kitu gani wakati mimi nilienda kumtafutia vitu kwajili ya show na vitu vyake mwenyewe. Kwahiyo akampigia simu mama ‘oooh mimi anifanyia dharau sijui nini mimi namuacha’ Mama yangu akamwambia ‘mbona unachukua jukumu la nani, kwasasa hujui mwenzako anafanya nini huko’. Akanitumia message sijui ‘mhuni unatoka UK sijui unaenda wapi bila kuniambia’, nikakubali kosa ‘nisamehe ila ongea na mzee akufahamishe vizuri’, akiniambia ‘sitaki tuongee na baba sitaki kufanya nini na wewe’ mwenyewe sitaki kukusikia’,basi hivyo ndivyo ilivyotokea,” alisema Dida.
Hata hivyo Dida amesema kwasasa hamwitaji tena kimapenzi Q Chillah ila anammiss kimazoea kwakuwa waliishi pamoja na kuzoeana.
Amedai alijitahidi sana kutuma pesa kwa Q Chillah ili zimsaidie kuachana na matumizi ya madawa wa kulevya. “Kuna watu nilikuwa nawapa pesa ili wampe Q Chillah aachane na matumizi ya madawa ya kulevya,ila sikutaka watu wamwambie kama nimetuma mimi, pia kuna watu wanadai eti mimi ndio nimesababisha Q Chillah atumie madawa,” alisema Dida ambaye kwa sasa anamiliki kampuni ya Dida Entertainment.