Featured Posts

Sunday, July 13, 2014

WAGANGA WA KIENYEJI WATAPELIANA WENYEWE KWA WENYEWE, SOMA HII HAPA


UTAPELI   sasa  wachukua sura mpya mkoani Iringa bada ya baadhi ya  waganga wa  tiba asilia (Sangoma) kugeuziana  kibao  wenyewe kwa wenyewe kwa  kuanza  kufanyiana  utapeli wa kutisha  ikiwa ni pamoja na kujifanya maofisa wa  polisi na  kuwatapeli fedha  wenzao  zaidi ya 60.



Imedaiwa  kuwa  waganga  hao matapeli  wana mtandao wao na wamekuwa wakiwatumia askari  wasio na maadili ya  jeshi la  polisi kwa  kwenda  kuwatisha  waganga  wachanga kwa madai kuwa  wao ni maofisa wa  polisi na serikali ambao  wanafuatilia  leseni zao  za kazi na  kuwatisha  kuwa wanafanya kazi kienyeji  hivyo  wanapaswa kufikishwa polisi na wakiwa  njiani  wanawataka  kutoa  rushwa kati ya 300,000 hadi milioni moja ama kuingia nao makubaliano ya mkopo ya fedha hizo za rushwa  kabla ya  kuwaachia.

Katibu  wa  chama  cha wanganga  wa  tiba asilia  wilaya ya  Iringa Dr  Salum Kalolo (pichani) alithibitisha  jana  kuwepo kwa  utapeli  huo na  kuwatayari  chama chake kimeanza  kuchukua hatua ya  kuwasaka matapeli hao ambao tayari baadhi yao majina  yao yanafahamika na  wanaendelea  kusakwa  ili  kufikishwa katika  vyombo  vya  sheria.

Dr Kalolo  alisema  kuwa  awali  utapeli huo  ulikuwa  ukifanyika chini kwa chini  na ili kuwa ni  siri  ila kwa sasa  utapeli  huo  umeendelea  kufanyika wazi wazi na  tayari  kama  chama  kimeona ni tatizo  kubwa  ina iwapo  watanyamaza kimya madhara  yanaweza  kuwa makubwa  zaidi .

" Tunasikitika sana  kuona  kuwa  waganga  wa tiba  asilia wameacha kufanya kazi  yao  ya uganga  na wamejiingiza katika wimbi  la utapeli  wa kuwatapeli  wanganga  wenzao fedha kwa kutumia njia ya  vitisho mbali mbali.....tena mbaya zaidi  wanawatumia baadhi ya  askari  kufanya  utapeli huo"

Alisema kuwa  waganga  hao matapeli  wamekuwa  wakijipachika  vyeo  mbali mbali zikiwemo  vya polisi na  maofisa wa  serikali  kupitia  wizara ya afya kwa madai  wametoka makao makuu na  wapo  mkoani hapa kwa ajili ya kufanya ukaguzi  mbali mbali kwa  waganga wa  tiba asilia jambo ambalo si kweli bali  wamelenga  kujipatia  fedha kwa  njhia ya udanganyifu

Dr Kalolo  alisema  kuwa  tayari  waganga  zaidi ya 60  wametapeliwa katika Manispaa ya  Iringa , Kilolo  ,Iringa  vijijini na wilaya ya  Mufindi na kuwa  wao kama  chama  wamekwisha wakamata  baadhi ya  wanganga  hao na pindi  wanapowafikisha  polisi  wamekuwa  wakiachiwa  huru .

Hivyo  ameliomba  jeshi la polisi na  serikali ya  wilaya na mkoa  kusaidia  kukomesha utapeli huo ili  kuepusha madhara zaidi  kujitokeza mkoani Iringa.

Mbali ya  kuomba  jeshi la polisi na serikali  kusaidia  kukomesha tabia hiyo pia  alisema hatua ambayo chama  chake  kimechukua ni pamoja na kuendesha zoezi la  kuyaondoa barabarani na mitaani  mabango yote ambayo  yamewekwa na  waganga  hao  wasio  fahamika .

 Wakati  huo  huo  chama   hicho  cha  wanganga  wa  tiba  asilia wilaya ya  Iringa  kimeiomba serikali kuangalia  uwezekano  wa  kutenga bajeti  kifedha  kwa ajili ya wanganga  hao  kupitia   vyama  vyao  ili  kuendelea  kuboresha  zaidi huduma  yao .
.
Kwani  alisema huduma  ambazo  wanganga  hao  wanazitoa ni kwawananchi wa Tanzania  hivyo  kama  ilivyo katika  sekta ya afya ambazo  zimekuwa  zimekuwa zikitengewa  bajeti.

TUMEAMIA HUKU