MH! Kigauni kifupi alichotinga staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven
Mengere ‘Steve Nyerere’ kimeibua minong’ono watu kuhoji kulikoni akivae hivyo ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
“Unajua siku zote tunaambiwa sisi Bongo Movie hatuna heshima, siyo kweli, kuna watu wapo kwa ajili ya kutudhalilisha. Angalia Wolper alichovaa,” alisema mwigizaji mmoja ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini. Alipoulizwa Wolper kuhusiana na madai hayo ya udhalilishaji, alijibu:“Achana nao hao ni wanafiki tu kwani kuna mtu amekatazwa kuvaa kama hivi?”





