Featured Posts

Wednesday, July 9, 2014

MSANII AMANDA AJITAPA KUPATA DUME LA MBEGU AAHIDI KUZAA MDA SI MREFU SASA

Na Gladness Mallya
STAA wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa mpaka sasa hajazaa kwa sababu bado alikuwa hajamuona mwanaume wa kuwa baba watoto wake.
Staa wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’
Akichonga na gazeti hili, Amanda alisema katika maisha yake anapenda sana mtoto lakini bado hajatokea mwanaume sahihi wa kuzaa naye ila anashukuru kwa sasa amempata.
“Miaka yote sijazaa kwa sababu nilikuwa sijamuona mwanaume sahihi wa kuzaa naye, lakini kwa sasa nimemuona japokuwa siwezi kumtaja kwa sababu bado naye nipo katika hatua za mwisho za kumpitisha kama anafaa,” alisema Amanda.

TUMEAMIA HUKU