Featured Posts

Saturday, September 20, 2014

Picha: Mpiga picha anaeiwakilisha Tanzania katika Big Brother Africa 2014, Muigizaji huyu wa kike anaweza kutajwa pia

Waandaaji wa shindano la Big Brother Africa
wameendelea kutangaza majina ya washiriki wa
shindano hilo, na leo wametaja majina ya washiriki
watatu akiwemo Idris kutoka Tanzania.
Kwa mujibu wa mtandao wa Big Brothe Africa, Idris
Sultani ameeleza kuwa ana mikakati na anatumaini
washiriki wenzake watamgeukia yeye pale
wanapotaka kuwa inspired au wanapokuwa katika
wakati mgumu.
Hata hivyo, taarifa za awali ambazo
hazijathibitishwa bado na waandaaji wa Big Brother
zilimtaja Idris Sultani na muigizaji Irene Veda kuwa
ndio watakaoiwakilisha Tanzania.
Baada ya Idris kutangazwa leo, taarifa hizo za
awali zimepewa nafasi zaidi. huenda Irine
akatangazwa hivi karibuni japo hakuna uhakika wa
kutosha.
Washiriki wengine waliotajwa leo kuwa kati ya
wanaowania ushindi katika shindano hilo lilopewa
jina la ‘Hot Shots’ ni Goitse kutoka Uganda na
Esther kutoka Uganda.

TUMEAMIA HUKU