Featured Posts

Saturday, September 20, 2014

Iran: Wafungwa miaka sita na bakora 91 kwa kucheza wimbo wa Pharrell 'Happy'

Kundi la wasichana na wavulana sita wa Iran
waliocheza wimbo wa Pharrell Williams ‘Happy’ na
kisha video yao kusambaa kwenye mitandao
mwezi May mwaka huu wamekamatwa tena rasmi
na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela na
bakora 91.
Hukumu hiyo inakuja ikiwa ni miezi kadhaa tangu
walipokamatwa kwa kosa hilo na kuachiwa kwa
muda baada ya watu mbalimbali duniani kukemea
kwa nguvu kitendo hicho kwa kuwa waliamini
vijana hao walikuwa wanajifurahisha tu.
Hata hivyo, kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa
kinyume na sheria za nchi hiyo hususani mavazi
waliyokuwa wamevaa na aina ya michezo
waliyoicheza.
Vijana hao walikiri kosa hilo na kueleza kuwa
walirubuniwa na watu kuwa ilikuwa sehemu ya
usaili wa kazi ya uigizaji jijini Tehran.
Muda mfupi baada ya hukumu hiyo kutajwa,
mwanasheria wa aliyekuwa anawatetea vijana hao,
Farshid Rofugaran ameeleza kuwa hukumu hiyo
imesamehewa kwa mujibu wa sheria na kwamba
itatekelezwa endapo vijana hao watarudia kosa
kama hilo ndani ya kipindi cha miaka mitatu.

TUMEAMIA HUKU