FAGIO! Mkali wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amemmwagia sifa shosti yake Wema Sepetu na kudai anafaa kuwa mke kama alivyo yeye.
Akimmwagia sifa mbele ya kinasa sauti chetu, Aunt alisema Wema anajua mapenzi ya dhati, anajali, mcheshi na anajua maisha tofauti na watu wengi wanavyofikiria.
“Siyo kwamba namsifia lakini Wema anafaa kuwekwa ndani, unajua watu wanashindwa kujua tu kwamba Wema nje ya ustaa wake anajua kuhimili maisha, anafaa kuolewa,” alisema Aunt. Wema na Diamond wapo katika mikakati ya kufunga ndoa |