Mshambuliaji Mario Balotelli mwenye umri wa
miaka 24, aliyehamia Anfield kutoka AC Milan kwa
Pauni milioni 16 mwezi uliopita, jana alitolewa nje
katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Wolves baada ya
kuzozana na refa, Chris Foy.
Balotelli akielekea nje baada ya mzozo huo
Bahati nzuri, alizuiwa na mchezaji mwenzake, Kolo
Toure wakati Foy akizungumza naye kwenye
mchezo huo.
Chanzo cha mzozo huo ni baada ya Mtaliano huyo
kugongana na mchezaji wa Wolves. Baada ya
mzozo huo tu, Balotelli alitolewa nje mara moja.
Kolo Toure (kushoto) akimzuia Balotelli asiendelee
na mzozo