Mzungu Kichaa amekanusha uvumi huo na
kusema hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi
na Salama.
“Sio kweli mimi si-date na Salama Jabir” Alisema
alipohojiwa na katika kipindi cha TV cha Sporah,
“tulifanya kazi pamoja kama majaji katika kipindi
cha TV (BSS), so kuna vitu vingi ambavyo
tunafanana pia alisoma UK na ni mtu mzuri, so ni
marafiki tu kulikuwa na uvumi ulisambaa kwenye
media”.
Salama Jabir
Pamoja na kuwa hakuna ukweli wowote juu ya
swala hilo lakini Mzungu Kichaa amedai kuwa kuna
mtu aliwahi kumuuliza kama ana uhusiano na
Salama na alimjibu ndio lakini hakumaanisha.
Mzungu Kichaa katika Sporah show
“kuna mtu aliniuliza nikiwa uwanja wa ndege,
Mzungu Kichaa ni kweli una uhusiano nae, ilinibidi
niseme ndio kwasababu nilikuwa nacheka sababu
ilikuwa ni idea ya kuchekesha kwamba Mzungu
Kichaa ana uhusiano na Salama.” Alisema Mzungu
Kichaa.
Akiuzungumzia uhusiano wake na Salama
amesema,
“Sisi sio best friends so sio kwamba tunatoka sana
pamoja, ninayo namba yake, na yeye lazima
atakuwa nayo ya kwangu lakini hatutumiani
ujumbe kila wakati.”
Katika hali ya utani mzungu Kichaa alisema:
“People thought it was really funny and they got
excited about it because imagine if these two, the
crazy white man and the crazy Salama, coz Salama
is crazy imagine if those two have children how
crazy they will be.”
Aliongeza kuwa baada ya kusikia
kinachozungumzwa mitaani aliwasiliana na Salama
kumjulisha,
“Nilimtumia barua pepe kumwambia kile
kinachosemwa na watu ili asije kushtuka akija
kusikia”.