Featured Posts

Friday, September 5, 2014

Gardner G Habash azungumzia tetesi za kuachana na Lady Jay Dee na chanzo chake,

Gardner G Habash amekanusha taarifa zilizokuwa
zimesambazwa kwenye mitandao kuwa yeye na
mkewe Lady Jay Dee wako kwenye wakati mgumu
wa ndoa yao.
Akizungumza katika Exclusive Friday ya 100.5
Times Fm, Gardner ameeleza kuwa hizo ni taarifa
zisizo za kweli ambazo amekuwa akizisikia tu.
“Hakuna tatizo. Kusema ukweli nimekaa na Lady
Jay Dee kwa miaka mingi sana na hii sio mara ya
kwanza kuzungumzwa kwa mambo kama hayo. Na
tumeshazoea. Hata kama kuna kitu
kinazungumzwa, mimi hata sina habari kwa
sababu nimeshazoea. Kwa hiyo na mimi pia
nimesikia kama ulivyosikia wewe. Lakini tatizo
hakuna.” Amesema Gadner.
Ameeleza kuwa chanzo cha tetesi hizo kinaweza
kuwa siku ambayo yeye alionekana polisi katika
kesi ya usalama barabarani na Lady Jay Dee
hakufika.
Amesema huenda watu walichukulia tofauti lakini
ukweli ni kwamba yeye ndiye aliyemshauri asiende
ili kuepusha attention zaidi.
“Na kwa watu kuzungumza…unajua Jay Dee ni mtu
mashuhuri, ni mkubwa sana. Kiasi kwamba kitu
kidogo tu kikitokea, hata akijikwaa kinazungumzwa
kwa ukubwa huo. Kwa mfano mimi nimepata shida
kidogo ya kesi ya traffic, kwa hiyo nikamshauri
mwenzangu asije pale polisi kwa sababu ya
kuogopa tu vitu kama mapicha na nini. Kumbe
watu walinotice kwamba hakuja. Kuanzia hapo ndio
ikaanza ‘aah kuna tatizo..kuna tatizo’.
“Lakini kwa kweli kuzungumzwa kwa msanii
mkubwa kama yule ni jambo la kawaida. Na ni
jambo ambalo ameshalizoea na mimi
nimeshalizoea pia.”
Hivo karibuni Jide alipost picha ya mkono
inayoonesha pete yake ya ndoa kumaanisha
uimara wa ndoa yao tofauti na kilichokuwa
kikisemwa.
jidejaydee
1826 likes 104 comments
Katika hatua nyingine, Gardner G. Habash ambaye
ni mtangazaji wa kipindi cha Maskani cha 100.5
Times Fm atafanya kipindi LIVE leo kutoka katika
eneo la Makumbusho Stand, Dar es Salaam akiwa
na timu nzima ya kipindi hicho.

TUMEAMIA HUKU