Kiungo wa klabu bingwa nchini Ufaransa Paris
Saint-Germain, Marco Verratti amevunja ukimywa
na kueleza namna anavyozihusudu klabu nguli
nchini Uingereza Man Utd pamoja na Arsenal.
Verratti ambaye ni sehemu ya kikosi cha timu ya
taifa ya Italia ambacho kinajiandaa na michezo ya
kuwania nafasi ya kufuzu kucheza fainali za barani
Ulaya za mwaka 2016, amesema ni kitambo
amekua akizihusudu klabu hizo za nchini
Uingereza.
Amesema pamoja na kuvutiwa na klabu hizo mbili,
pia ana anamini ipo siku atatimiza ndoto za
kuitumikia moja ya klabu hizo ambapo amesisitiza
kila unapofika wakati wa dirisha la usajili huwa ana
shauku ya kuona Arsenal ama Man Utd wanatuma
ofa ya kutaka kumsajili lakini huwa inakuwa tofauti.
Amesema kitu kikubwa kinachomshawishi
kuzitamani klabu hizo ni soka la ushindani
wanalocheza na pia wingi wa wachezaji wenye
vipaji vya hali ya juu waliopo nchini Uingereza.
Amesema ligi ya Uingereza pia inamvutia na
kufikia hatua ya kutamani kucheza kwenye ligi hiyo
siku moja ya maisha yake.
Lakini pamoja na yote hayo huenda ikawa vigumu
kwa Verratti kutimiza ndoto zake katika kipindi cha
karibuni kutokana na mkataba wa miaka mitano
aliosaini siku za hivi karibuni, hatua ambayo
itaigharimu kiasi kikubwa cha pesa klabu yoyote
itakayoonyesha lengo la kumsajili.
Marco Verratti alisajiliwa na klabu bingwa nchini
Ufaransa PSG, mwaka 2012 akitokea nchini kwao
Italia alipokuwa akiitumikia klabu ya Pescara
ambayo ilimkuza tangu mwaka 2000.