Mke halali wa Rais wa bendi ya mashujaa musica Charles Gabriel Cyprian ‘Chaz Baba’, Rehema Sospeter Marwa mwishoni mwa wiki jana alizua timbwili la mwaka baada ya kumchapa makofi msichana mmoja ajulikanaye kwa jina la Husna….
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwandishi wetu lilitokea majira ya saa nane za usiku katika ukumbi wa Letas ( zamani Busness Park) uliopo Makumbusho wakati bendi ya Mashujaa ilipokuwa inatoa burudani.
Sakata zima lilikuwa hivi;Husna alikuwa anakunywa kwenye Pub hiyo , mara akatokea mke wa Chaz Baba na kumfuata kaunta Husna na kumwambia amependeza sana kwa pamba alizotupia kisha akamuomba amsindikize chooni.
Wakati wanaongea, mwandishi wetu aliwasikiliza na kuanza kuwafuatilia hadi chooni. Walipofika chooni Rehema alimkunja Husna na kumwambia kuwa yeye ni mke halali wa Chaz Baba hivyo anamuomba aachane na mume wake lasivyo atamng’oa meno….
“Sikia nikwambie wewe binti, mimi ndo mke halali wa Chaz Baba, hivyo nakuomba kiustaarabu uachane na mume wangu lasivyo utahama mjini bila kupenda, “ alisikikia akisema Rehema huku akiwa amemkwida Husna.
Hata hivyo Husna alijitetea kwamba hana mahusiano na Chaz Baba kwani walishaachana muda mrefu na kumtaka Rehema asikurupuke….
“Nisikilize wewe mwanamke, siku nyingine usiwe unakurupuka kama kichaa, kuolewa unajiona umefika ee!! Sasa kwa taarifa yako huyo Chaz baba nilishamtema kitambo tu, achana na mimi, hangaika na wengine…..Kwanza jichunge wewe mwanamke,” alisikika akisema Husna.
Kauli hiyo ilimkera Rehema na kumtia Nakozi mbili za moto ( makofi mawili adimu) Husna aliyekuwa amevalia kigauni cha rangi nyekundu kisha akaondoka na kurudi kupata kilaji ndani ya Pub hiyo wakati mumewe akiendelea kutumbuiza….
Baada ya tukio hilo, mwandishi wetu alimfuata Rehema ambaye alikuwa na wapambe wa kutosha na kumuhoji kulikoni kupigana chooni..!!!!??
“Ndo ivo, nshamtandika vibao, nilikuwa nampa onyo aachane na mume wangu, ni hilo tu,” alijibu Rehema.
Husna aliporudi ukumbini alianza kuelezea tukio zima lilivyokuwa hadi kuchapwa makofi, “Mimi namshangaa sana yule mwanamke, yaani kiukweli Chaz Baba nshafanya naye mapenzi siku nyingi na nimeshaachana naye. Sasa namshangaa anakuja kuniuliza leo na kunipiga chooni, ila we acha tuu, kuna kitu ntamfanyia, asidhani namwogopa,” alisema Husna.