Featured Posts

Thursday, May 22, 2014

TAZAMA PICHA ZA KUSIKITISHA ZA MCHUNGAJI AMBAYE ALIMWAGIWA TINDIKALI NA KUHARIBIWA SURA

Mchungaji Umar Umulinde wa Uganda akiwa hospitalini.

Hizi ni baadhi ya picha alizopiga hivi karibuni mchungaji Umar Umulinde wa Uganda ambaye alimwagiwa tindikali katika mkesha wa sikukuu ya christmas mwaka jana mara baada ya kumaliza ibada,ambapo mpaka sasa kikubwa ambacho mchungaji Umulinde ambaye alikuwa muumini wa dini ya kiislamu kabla ya kubadili na kuokoka anasema ni kwamba waliomwagia tindikali ni waumini wa dini yake ya zamani kwani kabla ya kumwagiwa huyo mtu alisema neno linalotumiwa na waumini wa dini hiyo,ingawa kumekuwa na kuhusishwa kwa watu wengine kuhusiana na tukio hilo ingawa mchungaji huyo hataki kuamini.
sura yake ndivyo inavyoonekana kwasasa.
Mchungaji Umulinde.

Ambapo mpaka sasa amekuwa akiuliza maswali mbalimbali kuhusiana na allah na Mungu wa biblia kama wana uhusiano wowote kwamaana Mungu wa biblia anayemuamini aruhusu mtu kuua ili akarithi mbingu kama allah anavyotaka,zaidi amewashukuru watu wanaoendelea kumuombea na kumtembelea hospitalini Kampala international ambako amelazwa akiendelea na matibabu pia sasa amewataka waumini wa dini ya kikristo kuendelea kuwaombea wenzao ili wamjue Mungu wa kweli kuliko kuendelea na malumbano nao kwakuwa hakutakuwa na faida yoyote.
 


 


 
Mchungaji Umulinde akiwa nje ya hospitali kupunga upepo,picha juu baadhi ya marafiki waliomtembelea hospitalini.


 
Mchungaji Umulinde kabla hajakumbwa na tukio la tindikali


 
Hapa akiwa kwenye moja ya mikutano aliyoiendesha nchini Uganda.

Mchungaji Umar Mulinde akiwasili uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda.

Hatimaye hali ya mchungaji Umar Mulinde wa nchini Uganda ambaye aliharibika sura kwakumwagiwa tindikali usoni na watu wanaodaiwa kuwa ni waumini wa dini ya kiislamu wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi mwaka 2011 ikiwa ni adhabu kwa mchungaji huyo kwa kubadili dini, sasa anaendelea vizuri. 
Mchungaji huyo ambaye alikuwa mfuasi mzuri wa dini ya kiislamu huku baba yake akiwa ni imamu wa msikiti nchini Uganda, alipatiwa matibabu nchini kwake kwa takribani mwezi mzima toka apatwe na tukio hilo, kisha kupelekwa nchini Israel kwa matibabu zaidi, ambapo sasa hali yake imeimalika na kurejea nchini kwake kuendeleza kanisa lake. 

Mchungaji Mulinde Umar picha za mwanzo baada ya tindikali.

TUMEAMIA HUKU