Featured Posts

Sunday, May 11, 2014

STEVE NYERERE AMPA WEMA MAKAVU LIVE


MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo Movie Unity,
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameibuka na
kumuonya Wema Sepetu kupiga kazi na kuepuka
umaarufu bila kazi.
Nyerere amemtaka Wema aachane na skendo za
kila kukicha kwani hazina maana kama kazi ya
sanaa aliyoichagua kama njia ya kumuingizia
kipato.
“Kwanza nampongeza sana Diamond kwa tuzo
zote alizopata kwa kuwa alistahili lakini Wema
naye anapaswa kuiga mfano, vinginevyo atakuwa
maarufu bila ya heshima,” alisema Steve
Nyerere.

TUMEAMIA HUKU