Nyota wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya madaktari ambao hawakutaka majina yao yatajwe kwa madai kwamba msemaji wa hospitali hiyo ni mganga mkuu zinaeleza kwamba, mwanamuziki huyo anaendelea vizuri kiafya tofauti na tetesi za mitaani kwamba amerudia kubwia unga.
Uwazi lilimtafuta Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Sophinias Ngonyani ambaye alikiri Ray C kuhudhuria kliniki ya hospitali yake na kutakiwa kumaliza muda aliopangiwa wa miaka miwili na endapo atakatisha atadhurika.
“Hapa hospitali mbali na Ray C, kuna waathirika wengine nao wamekuwa wakihudhuria kliniki na wanaendelea vizuri.
“Hata hivyo, Ray C amebakiza miezi michache, tumemwambia asithubutu kukosa kufika kliniki hata siku moja hadi amalize siku zake 730,” alisema mganga mkuu huyo.