Featured Posts

Thursday, May 22, 2014

HATIMAYE MCHUMBA WA KUAMBIANA AIBUKA LIVE! ALIFAHAMIANA NA MAREHEMU KUAMBIANA TANGU MWAKA 2006

MAMBO yameanza! Siku mbili tu baada ya mazishi ya mwigizaji na mwongoza filamu mahiri Bongo, marehemu Adam Kuambiana, mrembo mmoja ameibuka na kusema alikuwa mchumba wa marehemu.
Mrembo anayejulikana kwa jina la Lulu Jumanne ‘Selina’.
Kwa mujibu wa mrembo huyo, Lulu Jumanne ‘Selina’, alifahamiana na marehemu Kuambiana mwaka 2006 akamwambia ndoa yake haipo sawasawa.
Alisema walianzisha uhusiano lakini haukuwa wazi katika jamii. Alisema siku moja akiwa anaishi Mwananyamala, wazazi wake walimtembelea.
“Nikiwa na wazazi nilimwona Kuambiana anapiga hodi, akaingia akiwa na  begi la nguo. Niliogopa kwani wazazi walikuwepo na walikuwa hawamtambui.
Lulu Jumanne ‘Selina’, akiwa na marehemu Kuambiana.
“Hata hivyo, walielewa yakapita, tukawa tunaishi wote nyumbani kwa kupika na kupakua,” alisema Selina ambaye naye ni mwigizaji.
Aliendelea kuweka wazi kwamba, baada ya hapo maisha yaliendelea lakini ikafika mahali marehemu akahamishia mapenzi kwa Mbongo Fleva, Stara Thomas yeye akawa ‘zilipendwa’.
Akizidi kuanika mambo kuwa mwaka jana Kuambiana alirudi kwake baada ya kutofautiana na Stara, akataka waendelee na mapenzi yao.
Katika mahojiano mafupi kati ya Selina na paparazi, mambo yalikuwa hivi:
paparazi: Mlikuwa na mipango gani ya maisha?
Selina: Mingi tu. Kwanza alishanitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake na wadogo zake.
paparazi: Marehemu alionesha upendo wa dhati kwako?
Selina: Sana tu, kwani alipenda kuniita mke wake. Alikuwa ananiheshimu hadi mwisho. Hakuwa akipenda mwanaume anizoee.
paparazi: Unajua nini kuhusu kuumwa kwake?
Selina: Najua alikuwa anaumwa tumbo kwa muda mrefu. Alikuwa akila chakula cha maelekezo ya daktari.
paparazi: Mara ya mwisho ulizungumza naye nini?
Selina: Nilimshauri anunue simu yenye WhatsApp kwani mara nyingi Kuambiana alikuwa hapatikani hewani. Alikuwa hawezi kukaa na simu kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Selina alisema hapendi kueleza mengi lakini anaamini yeye ndiye mwanamke wa mwisho katika mapenzi na marehemu.


credit:gpl

TUMEAMIA HUKU