Featured Posts

Saturday, May 24, 2014

DAH DHARAU ZINGINE HUWA HAZINA FAIDA..ONA HUYU DADA ALIVYOADHIRIKA

Leo Asubuhi Nikiwa Ubungobus terminal....
Leo asubuhi nikiwa stand ya mabasi ya ubungo,mdada mmoja wakati anapanda kwenye kagari kake akadondosha simu.Mimi nikamuita ili nimweleze kilichotokea,akanisonya tena msonyo wa dharau sana na nikajuta kumgusa bega kwasababu ya kibao alichonipiga.
 

Alipoondoa gari nikaiokota hiyo simu na kuondoka zangu,wala sikuizima.



Nafika town simu hiyo ikaita nikapokea kwa shauku ya kujua nani,haya ndo ya kawa maongezi yetu na mpigaji.
 

Mimi; Hallo habari yako
 
Yeye; Nzuri
 
Mimi; nani wewe 
 
Yeye; Mimi ndo mwenye hiyo simu ....
 
Mimi; Na mimi ndo nilokuita na ukanizaba kibao Pale stand ya ubungo leo na ukanisonya
 
Yeye; Basi kaka nisamehe naomba unambie ulipo nije tuelewane 
 
Mimi; Nitakwambia baadaye (nikakata simu na kuzima)
 

Swali nimwambie napatikana wapi au nimpotezee ili liwe fundisho kwake?

TUMEAMIA HUKU