Featured Posts

Friday, May 23, 2014

ANJELINA JOLIE WA BONGO ATESWA NA BIFU LAKE NA KUAMBIANA

Stori: Shani Ramadhani
MKALI wa filamu za Bongo, Irene Paul ameweka wazi kuwa anateswa na bifu lake na marehemu Adam Kuambiana kwani amefariki dunia wakiwa wamekorofishana.
Mkali wa filamu za Bongo, Irene Paul
Irene alisema alitofautina na Kuambiana alipokuwa akiigiza Sinema ya Broken Family, miezi kadhaa iliyopita lakini hadi jamaa huyo anapatwa na umauti, hawakuwa na maelewano.
“Mimi nilikuwa na hasira, marehemu pia. Tukapishana kauli na kurushiana maneno makali, nawashauri wasanii tuache bifu maana kama hivi kifo kimemkuta ikiwa bado hatujapatana, namuombea lakini pia anisamehe huko aliko,” alisema Irene.

TUMEAMIA HUKU