Kamishna
wa jeshi Polisi katika mji wa Kwara nchini Nigeria Mr Ambrose
Aisabor,amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa wawili miongoni mwa
wengine, waliokuwa wakijishughulisha na uuzaji wa viungo vya binadamu.
Akihojiwa
na waandishi wa habari kamishna Ambrose alisema watuhumiwa Amos Kareem
na Abubakar Ladan,walikamatwa kufuatia msako mkali ulio endeshwa na
jeshi hilo na baada ya kuhojiwa kwa masaa kadhaa watuhumiwa walikiri
kuhusika na tukio hilo.
Aidha kamishna Ambrose amesisitiza kuwa jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa wengine.
Mmoja
wa watuhumiwa, Abubakar Ladan, aliuambia mtandao wa Vanguard kwamba
alikuwa ameahidiwa kupewa pikipiki kama angeweza kumpataia mteja wake
kichwa, mkono na mguu wa binadamu. kwa mujibu wa mtuhumiwa , alidai kuwa
nia ya yeye kufanya hivyo ni kutimiza ndoto yake ya kumiliki pikipiki
hicho ndio kitu kilicho msukuma aende makaburini kufukua maiti na kukata
kichwa,mguu na mkono kama inavyo onekana kwenye picha.
Mtuhumiwa
wapili ambae ni Amos Kareem wakati akihojiwa alisema kuwa wateja
wakubwa wa viungo hivyo ni wanasiasa na amesha wauzia mara
nyingi,mtuhumiwa huyo alikataa kata kata kuwataja wanasiasa hao kwa
majina kwa sababu za kiusalama dhidi yao.