Dida
Shaibu, mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani amefunguka
Exclusively kupitia Sunrise ya 100.5 Times Fm inayoongozwa na Fadhili
Haule na kueleza chanzo cha ndoa yake na Ezden ‘The Rocker’ Jumanne
kuvunjika. Ndoa iliyodumu kwa muda wa mwaka mmoja tu.
Dida
ameeleza kuwa mzizi wa tatizo lililopelekea ugomvi mkubwa kati yao ni
simu ya mkononi ya mumewe huyo wa wazamani baada ya kutaka kuitumia
kucheza game na kugundua kuwa imewekewa password kwa mara ya kwanza
katika uhusiano wao.
“Tatizo
kubwa la ugomvi wangu na X-Husband, tatizo kubwa lilikuwa ni simu.
Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumatano tumetoka kazini. Tukawa tuko kawaida,
unajua sisi huwa tunataniana sana. Kwa hiyo aliacha simu yake
kitandani, unajua mimi huwa nacheza game kupitia simu yake. Kwa hiyo
mimi nikachukua simu yake nikakuta ameweka password kitu ambacho sio cha
kawaida. Kwa hiyo mimi ikabidi nimuulize…nikamuita, tulikuwa tunaitana
‘mshikaji wangu mshikaji wangu’. Kwa hiyo alikuwa yuko bafuni anaoga,
kwa sababu nyumba ni self-contained, kwa hiyo nikawa namwambia ‘duh
mshikaji wangu mbona umeweka password?’ yaani kama utani tu, akaniamba
‘aah we iache simu yangu’.” Dida ameiambia Sunrise ya Times Fm
Amesema
Ezden alishikilia msimamo wake kutomuonesha password kitu ambacho
kilimpa hisia na wasiwasi kuwa huenda jamaa anamsaliti (anamichepuko)
ameficha kupitia simu hiyo na kuanza kuongeza nguvu ya kuomba apewe
password ili aondoe wasiwawasi wake lakini hakufaulu zoezi hilo.
Ameiambia
Sunrise ya 100.5 Times Fm kuwa kitu kilichomfanya afikirie kuwa
ameonewa kwa kunyimwa password ni uhuru aliokuwa nao mumewe huyo wa
zamani kupitia application za kidijitali.
Amesema
Ezden alikuwa na uwezo wa kuona kila kinachofanyika kwenye simu ya Dida
hata kupata jumbe zinazoenda kwenye simu ya Dida kabla mwenyewe
hajazipata
“Simu
yangu anauwezo wa kushika akakaa nayo, simu yangu anaweza kushika
akadownload vitu vya kuweza kufatilia Dida anaenda wapi, Dida anafanya
nini. Messages zangu za WhatsApp alikuwa anaweza kupata yeye kabla yangu
mimi. Na kingine kikubwa ni kwamba alikuwa anaweza kudownload maongezi
ambayo naongea na watu. Lakini hajawahi kukuta maongezi mabaya na
watu….Nikiwa Kawe simu yake inamuonesha kuwa Dida yuko Kawe.” Ameeleza.
Hata
hivyo, ametaja kuwa wasiwasi wa mumewe huyo wa zamani na mabadiliko
yake katika matumizi ya simu yalitokana na ujumbe ambao alikuwa
ametumiwa na mwanaume ambaye kwake yeye ni mteja.
Lakini
ujumbe huo haukueleweka vizuri kwa sababu kuna kitu anadhani kilimiss
kwenye ujumbe huo kilichosababisha ieleweke tofauti (Kama mtu
anaechepuka nae).
Ameeleza
kuwa alipoendelea kuomba zaidi password na hali ya kutoelewana
kuongezeka akajikuta akipigwa vibao na hapo mambo yakazidi kuwa mabaya
kwenye uhusiano huo.
“Alinipiga
kibao, sio kibao tu, Vibao vya uhakika….baada ya kupigwa mimi
nilishikwa na hasira kwa sababu alinipiga na baadae akaona kibao
hakitoshi. Akachukua mkanda, mkanda huu wenu wa suruali lakini ulikuwa
mzito akawa ananichapa nao ‘kwa nini unataka kupishika vitu vyangu’.
Anasema
kutokana na kipigo hicho aliumia kichwani na kuelekea hospitali, lakini
aliporudi nyumbani alikuta mwenzake ameshachukua vitu vyote alivyokuwa
anavimiliki (alivyoenda navyo).
Alipoulizwa nani alimuacha mwenzake:
“Sitaki
kusema nani kamuacha mwenzake kwa sababu mimi ndiye niliomba divorce.
Katika maisha ya mwanadamu wanasema mwanamke hauwezi kumuacha mwanaume
ila mwanaume anaweza kumuacha mwanamke. Lakini mimi nahisi kama
tumeachana.”
Katika
hatua nyingine, Dida aliulizwa kuhusu mpango wake wa baadae katika
uhusiano wake kama ana mpango wa kuolewa tena. Alisema hana mpango huo
kwa sasa.
“Kwa
sasa sina mpango wowote wa kuhusiana na suala la ndoa. Yaani sina na
sitegemei. Na kama kuna mtu anafikiria kwa sababu napata maombi mengi
sana. Washindwe na walegee. Kwamba labda naweza kusema mwenyezi Mungu
amenijalia kuwa nabahati hiyo…Sio kupendwa yaani tuseme, unajua binadamu
anakupenda mwingine anakujaribu. Sasa hivi watanifuata wanaume wengi
sana kila mmoja atakuja kwa sampuli anayoijua yeye. Huyu atajifanya yeye
ndiye ana mahaba kuliko Yule. Mwingine anasema ‘atapigaje mwanaume?’
kumbe yeye ndiye mdundindaji kwelikweli kuliko hata yule.
“Sitaki
kuja kujutia maisha yangu, sitaki kuja kujutia maamuzi yangu. Huwa
nafanya kitu kwa kuangalia mbele zaidi. Mimi nina biashara zangu, nina
maisha yangu. Namshukuru Mungu amenijalia mtoto mmoja. Kwa hiyo nahitaji
mtoto wangu awe na maadili fulani hivi ambayo ya kusema kwamba huyu ni
mama..nahitaji kumsomesha, nahitaji awe hivi. Lakini sitaki mwanangu
asipate matatizo haya ambayo labda mama yake nimepitia. Lakini hii yote
nasema ni ujasiri. Nasema Mwenyezi Mungu labda ananionesha njia.”
Source:Times FM
Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam
-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392
milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa
ajili y...