Featured Posts

Friday, July 4, 2014

MAKAVU LIVE: TABIA MBAYA YA WASTARA...ALIMKOSEA SANA MAREHEMU...!ACHANWA LIVE...!

 BIG boss wa Kampuni ya Five Effect, William Mtitu
BIG boss wa Kampuni ya Five Effect, William Mtitu amemtolea uvivu msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma kwa kumwambia kuwa, alimkosea sana marehemu Sheila Haule ‘Recho’ kwa kutomzika.

 Akizungumza na mwandishi wetu, Mtitu alisema marehemu Recho alikuwa mtu wa kujitoa katika matatizo mbalimbali ukiwemo msiba wa mume wa Wastara, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ lakini alishangaa kutomuona kwenye msibani huo na alipomchana laivu akakasirika na kutangaza bifu.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Wastara, Juma
 “Nilimchana laivu kwani alimkosea marehemu, alipaswa kwenda kwani hakuwa na sababu ya kueleweka zaidi ya kwenda bungeni kitu ambacho angeweza kukiacha kikawakilishwa na mtu mwingine,” alisema Mtitu.Kwenye utetezi wake juu ya kutoonekana msibani, Wastara alisema hakuwa na jinsi kwani alikwenda bungeni mjini Dodoma kuwawakilisha wasanii wenzake.

TUMEAMIA HUKU