Kupitia mitandao na magazeti siku chache
zilizopita ilitoka stori ambayo ilidai Kajala
anaelekea kumuajiri Wema Sepetu,leo Wema
kapatikana na kakubali kuongelea isue hizo zote
ikiwemo hiyo ya Kajala.
Kupitia You heard ya XXL ya Clouds Fm Soudy
Brown alianza kwa kutaka kufahamu kama kweli
Kajala anaweza kumuajiri yeye[Wema],Wema
Sepetu akamjibu>>’Inawezekana,kila kitu
kinawezekana Soudy’
Kuhusu mshahara ambao anataka kulipwa na
Kajala,Wema Sepetu amejibu>>’Kwa Kajala mi
sihitaji mshahara hata bure nitafanya kazi kwa
Kajala,shughuli yoyote nitafanya Soudy’
Soudy Brown alipomuuliza kuhusu fununu za
Meninah kutoka na Diamond,Wema
amejibu>>’Mimi sijui Soudy bwana na wala
sijali’.