wakati mkisubiria ya Diamond na Wema, huko Hollywood kimeshanuka.
Wakati watu wakizidi kusubiria tukio la kihistoria kwenye sanaa ya Bongo fleva na bongo movie, ndoa kati ya Diamond Platnumz na Wema Sepetu kufunga ndoa, huko Hollywood hiki ndicho kilichojiri. Ni baada ya miaka tisa ya mahusiano hatimaye imekuwa, huko hollywood weekend hii hii haya ndio yaliyo-make headlines, ni harusi kati ya ma-star wakubwa wawili Angeline Jolie na Brad Pitt, wawili hawa walififanya harusi ndogo iliyoalika wana ndugu tu wa karibu na marafiki, harusi iliyofanyika katika mji wa Chateau Miraval, Hii inakuwa ni ndoa ya pili kwa Brad Pitt na ya tatu sasa kwa Angeline Jolie.