MSIKITI wa madhehebu ya Wahindu uliopo maeneo ya Mtaa wa Kibasila karibu na shule ya Olimpia jijini Dar es Salaam, umeteketea kwa moto leo asubuhi ambapo baadhi ya mali zimeungua na mtu mmoja kukimbizwa hospitali kutokana na mshituko.
Akizungumza na mtandao huu, shuhuda mmoja alisema moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye mashine ya luku ambapo baadhi ya waumini walikuwa wakijiandaa kuupamba msikiti huo.