Featured Posts

Monday, September 15, 2014

NOMA SANA HII, MCHAWI ADONDOKEA KANISANI, AZUA TAHARUKI KANISANI

NIkweli imetokea! Ni kwenye Kanisa la Paradise Internation Ministries lililoko Karakata Ukonga jijini Dar, mwanamke mmoja (pichani) anayedaiwa mchawi alidondoka usiku wa saa saba na kujikuta hawezi kutembea.
Mwanamke anayedaiwa kuwa mchawi akiwa amedondoka Kanisani.
Tukio hilo lilijiri Septemba 13, mwaka huu wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa wamezama kwenye maombi ya kufunga.
Ilidaiwa kuwa, waumini wa kanisa hilo wakiwa katika maombi hayo, Nabii Gideon Parapanda aliwahakikishia kuwa usiku huo kutatokea mambo ya ajabu kufuatia maombi hayo.
Inadaiwa ilipofika saa saba usiku mwanamke huyo akiwa na wenzake watatu, walidondokea kanisani hapo na kusababisha taharuki kwa waumini waliokuwa wakifanya maombi ndani. Mwanamke huyo alikuwa na kitambaa chekundu kikidaiwa ni hirizi, fimbo  nyeusi iliyozungushiwa shanga na alikuwa amejipaka masizi mwilini.
Mwanamke baada ya kudondokea kanisani na kusababisha taharuki kwa waumini waliokuwa wakifanya maombi ndani. 
Akizungumza na Uwazi, Nabii Parapanda alisema watu hao walidondoka watatu, wawili walifanikiwa kukimbia akabaki huyo mmoja aliyejitambulishwa kwa jina moja la Aisha, mkazi wa Mwananyamala A jijini Dar.
Baada ya tukio hilo vyombo vya ulinzi, askari wa JWTZ na polisi walifika kwa lengo la kuhakikisha usalama wa eneo  hilo lakini nabii huyo aliomba mtu huyo asichukuliwe hadi atapofanyiwa maombi maalum.
Ombi la kiongozi huyo lilikubaliwa ambapo Aisha alipandishwa  madhabahuni na kukiri kuwa alikuwa na wenzake watano lakini katika kuanguka walikuwa watatu, wawili walifanikiwa kukimbia bila kusema walikuwa wakitoka wapi kwenda wapi.
Kitambaa chekundu alichokuwa nacho mwanamke huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema:
“Ni kweli tukio hilo limetokea na watu wameshuhudia, mwanamke huyo bado  yuko kanisani hapo kwa maombi.

TUMEAMIA HUKU