Featured Posts

Saturday, September 13, 2014

MAKALIO YA LINAH NA RECHO YAWA KIVUTIO KWA WASUKUMA WA SHINYANGA FIESTA JANA, TAZAMA HAPA

Linah akiwa na madansa wake wakifanya yao jukwaani.
Staa wa wimbo wa Maumivu, Khadja akiimba sambamba na dada'ke Linah.
Khadja akiimba na mashabiki waliofurika ndani ya Uwanja wa Kambarage.
Rachel akiwa na madansa wake wakifanya yao jukwaani.
TAMASHA la Serengeti Fiesta 2014, usiku wa kuamkia leo lilifunika mbaya kutokana na mashabiki kibao kujitokeza kwa wingi ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage, Shinyanga ambapo kila msanii aliyepanda, alipata shangwe za kutosha.
Mpango mzima ulikuwa hivi, msanii wa kwanza kulitawala jukwaa alikuwa ni Mo Muziki, ambaye alipata shangwe za hatari na baadaye alishuka na kumkabidhi kipaza sauti mwanadada Khadja anayesumbua na wimbo wa Maumivu ambaye pia alikamua vilivyo na kumwachia jukwaa Recho kisha kumpisha Young Killer.
Makamuzi yalizidi kushika kasi baada ya Ommy Dimpoz kupanda jukwaani na kumkaribisha mrembo mmoja ambaye walijiachia vilivyo na kumpa pasi Stamina ambaye alikamua na kumuachia jukwaa Nay wa Mitego aliyempisha mtangazaji, Adam Mchomvu ambaye alimpandisha mwanadada Linah.
Shangwe zilikolea zaidi baada ya Mr Blue kupanda na baadaye kuwapisha Chegge na Temba ambao nao walifanya shoo kali na kumpisha Nikki wa II ambaye alifanya yake na kumpa kipaza Fid Q ambaye alifunga pazia burudani hizo.

TUMEAMIA HUKU