Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja
na miezi miwili , Regina Geofrey
ameuawa kikatili kwa kunyongwa na
baba yake mzazi Geofrey Kilngwa
‘Simbaiwe” (27) kwa kuwa alizaliwa
akiwa ameatanguliza makalio yake .
Baba wa binti huyo ambaye pia ni
mganga wa kienyeji anayeishi kitongoji
cha Mwikang’ombe, kijijicha cha
Katuma ,wilayani Mpanda alitenda
unyama huo kwa madai kuwa mtoto
aliyezaliwa kwa kutanguliza makalio yake
ni mkosi na nuksi kubwa katika shughuli
zake hizo za uganga wa kienyeji .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ,
Dhahiri Kidavashari akizungumza na
waandishi wa habari amedai kuwa mzazi
huyo aliyetenda uhalifu huo Julai 20
mwaka huu ambapo alikamatwa na jeshi
la Polisi Agosti 26, mwaka huu..
Inadaiwa siku hiyo ya tukio mtuhumiwa
huyo baada ya kumnyonga hadi kufa
binti yake huyo alimzika kwa siri katika
kibanda chake anachofanyia shughuli
zake za uganga wa kienyeji .
Akisimulia mkasa huo Kamanda
Kidavashari alidai kuwa mtoto Regina
alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa
ambao haukufahamika kwa zaidi ya
mwezi mmoja .
“Ndipo baba mzazi wa binti huyo
alipolazimika kuanza kumuuguza kwa
siri pasipo mama yake mzazi kufahamu
kwani alimdanganya kuwa mtoto wao
huyo amepelekwa kutibiwa na babu yake
huko mkoani Mwanza “ alieleza
Kidavashari .
Inadaiwa kuwa kibanda ambacho
mtuhumiwa alikuwa akifanyia shughuli
zake za uganga kilikuwa mbali na
makazi yake hivyo ilikuwa rahisi
kumficha mtoto wake huyo kwa zaidi ya
mwezi mzima akimtibu bila mama mzazi
wa mtoto huyo kufahamu .
Kwa mujibu wa kamanda
Kidavashari ,wakazi wa kitongoji cha
Mwikan’gombe wakiongozwa na
Mwenyekiti wao walimtilia shaka
mtuhumiwa kutokana na tetesi
zilizozagaa eneo hilo kuwa mtoto Regina
alikuwa ameuawa na baba yake mzazi na
kuzikwa kwa siri .
Inadaiwa wakazi hao na mwenyekiti
wao waliamua kufika nyumbani kwa
mtuhumiwa na kuhoji alipo binti yake
Regina ambapo alipinga vikali lakini
alipopekuliwa kibandani kwake
walibaini kuweko kwa tuta dogo
lililokuwa limechimbwa siku za
karibuni .
Kidavashari aliongeza kuwa wakazi hao
wakiongozwa na mwenyekiti wao
waliamua kufukua tuta hilo na kukuta
kichwa cha mtoto huyo kisha
wakaitaarifu polisi .
Mama ya marehemu aitwae Maria
Exavery (22) alidai kuwa hakuhusishwa
wala kupewa taarifa kwamba binti yake
huyo amekufa “Mie nilikuwa nafahamu
kuwa Regina yuko kwa babu yake ,
Mwanza akitibiwa “ alieleza .
Nae Regina Kaboni (40) mkazi wa Isamilo
Mwanza ambaye alikuwa akitibiwa na
mtuhumiwa anadai kuwa alishirikishwa
katika maziko ya binti huyo
“Hata hivyo nilishtushwa sana kwa
kitendo cha mtuhumiwa kumzika
mwanae bila ya kumshirikisha mkewe ,
nilipomuuliza mtuhumiwa alidai kuwa
kwa mila ya kwao mtoto aliyezaliwa kwa
kutanguliza makalio yake mama mzazi
wa mtoto ni mwiko kushirikishwa katika
maziko ya mtoto huyo ” anadai
Kwa mujibu wa Kidavashari watu wanne
wakiwemo wazazi wa marehemu
wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa
mahojiano zaidi ambapo watafikishwa
mahakamani mara tu baada ya upelelezi
wa awa;li kukamilika ..
Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi hilo ni
pamoja na Regina Kaboni na Msolwa
Jacob (29) mkazi wa kitongoji cha
Mwikanga’ombe .