KITUKO! Msanii wa sinema za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ ametoa kali ya aina yake kwa kusema anapenda ujauzito kiasi cha kufikia hatua ya kujaza matambara tumboni ili awe na muonekano wa mjamzito.
Msanii
Akizungumza na paparazi wetu, Koleta alisema kwa jinsi anavyopenda ujauzito,akimuona mwanamke yeyote mjamzito anamfuata na kuzungumza naye hata kama hamfahamu na kama yuko jirani ataenda kukaa naye.