Featured Posts

Tuesday, September 2, 2014

KAJALA.NAE HATIMAYE.AANDIKIWA BARUA YA WAZI NA WADAU ISOME HAPA

Kwako Kajala Masanja. Bila shaka ni mzima wa
afya. Binafsi mimi niko poa na ninaendelea na
majukumu yangu kama kawaida.
Leo nimekukumbuka kupitia safu hii , nataka
kuzungumza na wewe, na hasa katika suala
zima la ‘ ku - maintain’ ustaa wako . Ninaposema
ustaa wako , namaanisha heshima , kipaji (kazi)
pamoja na mapato yako.
Juzi kupitia gazeti la Ijumaa Wikienda
tumeona jinsi gani umepiga hatua kimaisha.
Umetoka katika maisha ya kuonekana wa
kawaida, sasa unapewa heshima ambayo
sidhani kama uliwahi kuitegemea kama
unaweza kuipata .
Ulikuwa mtu wa karibu na aliyekuwa shosti
wako , Wema Sepetu ‘ Madam’ ambaye wakati
huo alikuwa ana mkwanja mrefu kuliko wewe,
jinsi fedha ilivyo mwana haramu kwa wakati
huo ilikuwa ikiwezekana kabisa Wema
akakutuma kitu, ukatii .
Jeuri ya fedha aliyoionesha Wema wakati wa
matatizo yako alipokutolea shilingi milioni 13 ,
inaonesha ni jinsi gani mwenzako alikuwa
vizuri kifedha. Akakuokoa kwenye kifungo na
wewe ukarudi uraiani. Unakumbuka vizuri hata
baada ya yeye kukutolea fedha hizo nini
kiliendelea katika maisha yenu , starehe
mwanzo mwisho.
Mlikuwa mkiongozana na timu ya watu katika
kumbi mbalimbali za starehe mkionesha jeuri
ya fedha . Najua unakumbuka Wema
alivyofanya mbwembwe na fedha nyingi
kumleta msanii wa Nigeria , Omotola Jalade
Ekeinde kuja kuzindua filamu yake ya Super
Star ambayo haijaingia sokoni hadi leo .
Kwa jeuri hiyo na nyingine nyingi alizokuwa
akizifanya Madam, hakuna ambaye aliwaza
kwamba siku moja ufujaji wa fedha unaweza
kubadilika na kuwa fedha za mawazo. Hakuna
aliyewaza kwamba wewe ambaye ulikuwa chini
yake ungeweza kuja kuwa juu yake.
Hakuna linaloshindikana chini ya jua na sasa
kibao kimegeuka, sasa fedha
imekutembelea. Heshima ile ambayo alikuwa
akiipata aliyekuwa shosti wako , unaipata
wewe. Hapo ndipo unapotakiwa kupatazama
kwa makini .
Kama umefanikiwa kufungua kampuni yako ya
kuzalisha filamu , iwekee misingi thabiti isije
kuyeyuka kama ilivyoyeyuka ya huyo
aliyekuwa shosti wako (Wema ). Tengeneza
mazingira ya kuzalisha kazi na kuziuza kweli
Watanzania waone kwamba kuna filamu bora
zinazalishwa kutoka katika kampuni yako.
Kuwa na fedha nyingi na kutokokuwa na
mipango mipya ya kuzizalisha, ni rahisi
kupotea na kurudi kule ulikotoka . Njia aliyopitia
aliyekuwa shosti wako iwe funzo kwako .
Chagua njia sahihi ili uendelee kuwa makini
katika maisha yako.
Asikwambie mtu , starehe za kupindukia huku
ukiamini ‘ bado zipo benki ’ ndiyo chanzo cha
wengi kuporomoka . Natumai sijachelewa
kuzungumza na wewe maneno haya
machache, yafanyie kazi ili usije kujifunika
shuka wakati kumekucha . Mungu akubariki !

TUMEAMIA HUKU