Featured Posts

Thursday, September 11, 2014

INAMAAANA KAJALA UNATAKA KUTWAMBIA HUKUJIFUNZA KITU KWA WEMA SEPETU

KAMA mwandishi, sijawahi kukutana na Kajala
Masanja na kufanya mazungumzo naye, lakini
kama mdau nimeona kazi kadhaa za muigizaji
huyu mwenye jina kubwa katika Bongo
Movie. Anajitahidi kuigiza na katika uhalisia
wake, huyu ni miongoni mwa wadada
wanaoweza kuibeba tasnia hii na kuifikisha
katika levo zingine za mbali na kuiletea sifa
nchi yetu .
Nimewahi kusoma simulizi juu ya maisha
yake, inasisimua sana, hasa alipokuwa
akizungumzia sakata lililosababisha yeye na
mumewe kukamatwa , kufikishwa mahakamani
na hatimaye kuhukumiwa jela. Amepitia
maisha yanayotosha kumpa mifano na
mafunzo mengi ya maisha .
Kama siyo shoga yake Wema Sepetu kumlipia
fedha za faini alipohukumiwa pale Kisutu
mwaka mmoja uliopita, hivi sasa tungekuwa
angalau tumeanza kumsahau Kajala , kama
ilivyo kwa mume wake Agostino Faraji .
Lakini unapomuona maisha anayoishi hivi
sasa, unashindwa kujizuia kujiuliza kama ana
chochote cha kujifunza na kujutia katika
maisha anayopitia , hasa katika matumizi ya
fedha . Wanaomfahamu vizuri wanasema hivi
sasa msichana huyu ana fedha za kutosha ,
kiasi cha kumfanya atembee akiwa na
wapambe, si unajua tena kibongobongo ?
Sijajua ni fedha kiasi gani , lakini unapomuona
msichana kama Kajala , anakwenda kumtunza
mtu burungutu la shilingi laki sita na ushee, ni
lazima ukubali kuwa anazo za kutosha .
Enzi za ujana wetu , tulizoea kuwaona watu
walioitwa Mapedeshee wakifanya madoido
hayo katika kumbi za starehe na kwenye
mikusanyiko. Na ninawakumbuka bado, akina
Fikiri Madinda , Juma Banatoz ‘ JB ’ , Papaa
Msofe, Muzamil Katunzi , Papaa Chosta ,
Hussein Makabyureta , Rama Mutoto ya
Ng’ ombe , Jack Pemba ‘ JP’ na wengineo wengi
wa enzi zao .
Sitaki sana kuingia kwa undani kujua nini
kimewasibu watu hawa kwa sasa, lakini
ushahidi wa mazingira unaonyesha jamaa
wamebadili staili ya maisha , bila shaka baada
ya kugundua walikuwa wanapotea , kwa
sababu walikuwa wanayanunua majina yao
kwa bei kubwa sana .
Shoga yake Kajala , Wema Sepetu , miezi
michache iliyopita naye alikuwa katika hali
kama hiyo , akitapanya fedha kwa staili ya
kutembea na wapambe wengi, huku
akigharamia matumizi yao , hata yale yasiyo na
msingi.
Simfundishi namna ya kutumia fedha zake,
lakini ni ushauri tu ambao anaweza kuufuata
au kuushiti . Pesa haitoshi . Anaweza kuziona
nyingi leo , lakini sidhani kama zinaweza kufika
kesho.
Katika kutengeneza maisha , kesho iko mbali
sana, lakini kwenye matumizi , kesho ni
kufumba na kufumbua tu.
Watu wenye fedha zao tunaowajua , hawana
ujuha wa kumwaga hela ovyo kwa lengo la
kujitangaza, badala yake kama kurudisha
sehemu ya hela kwa jamii , hula na watoto
yatima , wazee wasiojiweza na wakati
mwingine kuwapa mahitaji muhimu kama
vyakula na mavazi.
Kajala bado ni binti mdogo . Kuwa na shilingi
milioni 50 , 100 au bilioni moja siyo kufika, bali
ni mwanzo mzuri wa kutengeneza maisha ya
baadaye. Nimshauri awekeze katika kilimo ,
majengo au ufugaji , uwekezaji ambao baada
ya miaka michache , fedha zitaanza kutiririka
bila kikomo na hivyo kumpa uhakika angalau .
Hana sababu ya kujenga jina kwa sababu
tayari analo ila ana ulazima wa kujenga
maisha kwa vile hana . Sifa za kijinga ndiyo
zinazowasumbua sana wasanii , wanashindwa
kuyajenga maisha yao kwa pesa wanazozipata
kutokana na fursa mbalimbali wanazokutana
nazo .
Hela zinapokuja hazipigi hodi na uzuri wake
zinapoondoka , mwenye kuzimiliki anajua kuwa
zinaondoka. Kajala anamjua Bill Gates? Ni
tajiri wa kutupwa, lakini kila siku anakuwa mtu
wa kwanza kufika ofisini kwake, kuhakikisha
utajiri wake hauyumbi.
Leo mdogo wangu Kajala umepata mkondo
unautumia kutafuta sifa, badala ya kujijengea
misingi imara ya maisha yako ya baadaye!

TUMEAMIA HUKU